Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe
huku ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar.
.................................................
Makamu wa
kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema wananchi wa
Tanzania na Zimbabwe wanayo nafasi nzuri kukuza maendeleo yao iwapo fursa za kiuchumi na
biashara zilizopo zitazidi kuibuliwa na kufanyiwa kazi.
Maalim Seif amesema
hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe,
Charles Makakala aliyefika ofisini kwake Migombani kwa ajili ya kujitambulisha
baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Makamu wa
Kwanza wa Rais amesema mbali na nchi hizo kuwa na uhusiano wa kidugu, lakinia pia
ni wanachama wa Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), hivyo malengo yao
ya kiuchumi na kibiashara yanafanana.
Amesema hivi
sasa kuna Watanzania wengi wakiwemo kutoka Zanzibar wanaofanya biashara nchini
Zimbabwe, kama ilivyo kwa wafanyabiashara wa Zimbabwe nchini, hivyo ni dhahiri
mafanikio makubwa zaidi yatapatikana, iwapo mazingira ya kibiashara yataimarishwa
zaidi.
Naye Balozi
Makakala ameahidi kuwa atajitahidi kutekeleza diplomasia ya kiuchumi, na kuzidi
kuibua fursa zote za kiuchumi na kibiashara kwa azma ya kuimarisha mazingira
bora ya kufanya shughuli hizo kwa maslahi ya wananchi wa nchi mbili hizo.
Balozi
Makakala ametuliwa kushika wadhifa huo, baada ya mtangulizi wake, Balozi Adadi
Rajabu kumaliza muda wake na sasa ameingia katika harakati za kuwania nafasi ya
Ubunge katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
|
Post a Comment