Yaya Toure ang'ara Ushindi wa Man City
Yaya Toure aliiongoza Man City
katika ushindi mnono dhidi ya West Brom ambapo Raheem Sterling
aliyesajiliwa majira ya joto kwa dau la pauni milioni 49 akicheza mchezo
wake wa kwanza kwa timu yake mpya.
Mkwaju wa Toure uliombabatiza
mchezaji mwenzake David Silva ulikwenda pia kwenye miguu ya mlinzi wa
West Brom Craig Dawson kabla ya kutinga nyavuni.
City waliendeleza
kupanua ushindi wao baada ya Toure kupiga mkwaju mwingine uliokwenda
kona ya juu na kuwa goli la pili.Nahodha Vincent Kompany alihitimisha
ushindi huo kwa mpira wa kona na kuwa mwanzo mzuri katika dhamira ya
kulipata taji la ligi kuu.
West Brom walikua na nafasi chache
baada ya mpira wa kona uliopigwa na Chris Brunt kuunganishwa kwa kichwa
na James Morrison ambayo ilidakwa vyema na Joe Hart.
City watakua
wenyeji wa mabingwa wa amsimu uliopita Chelsea na inawezekana wakamkosa
kiungo Yaya Toure aliyetolewa baada ya kupata maumivu ya misuli ya paja.
Post a Comment