Mfumuko wa Bei wa Taifa Wapungua Nchini
Na Aron Msigwa - Maelezo
Waandishi wa Habari wakiwa kazini, wakati Ofisi ya Taifa ya Takwimu ikitangaza Mfumuko wa Bei Mwezi Machi 2016 leo. |
...................
Kuhusu Fahirisi za
Bei ambacho ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei ya bidhaa na
huduma zinazotumiwa na kaya binafsi hapa Tanzania kwa mwezi Machi, Kwesigabo amesema
kuwa zimeongezeka hadi kufikia 101.93 kutoka 101:44 za mwezi Februari.
Amesema baadhi ya bidhaa za vyakula za vyakula zikiwemo unga
wa muhogo, matunda, maharagwe na samaki zimechangia kuongezeka kwa Fahirisi
hizo na kuongeza kuwa bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia ongezeko hilo ni
Mavazi ya wanawake, mkaa na kuni.
Kwa upande wa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika
kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa mwezi Machi , 2016 umefikia shilingi 98 na senti 11 ikilinganishwa na uwezo wa shilingi 98 na senti 58 wa mwezi Februari
2016.
“Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania
katika kununua bidhaa na huduma zilezile kwa mlaji kwa mwezi Machi 2016
umepungua, hii ina maana kuwa sasa mtu kuongeza ziada ili aweze kununua bidhaa
na huduma sawa na zile alizokuwa na uwezo wa kuzinunua mwezi Februari"
Kwa upande wa
mfumuko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki mwezi
Machi, 2016, Kwesigabo amesema una mwelekeo unaofanana; Kenya umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 6.45 kutoka 6.84
huku Uganda ukifikia asilimia 6.2 kutoka asilimia 7.0 za mwezi Februari.
Post a Comment