Tigo, Mgahawa wa Samaki Samaki waingia Ubia
................
Kampuni ya simu inayoongoza kwa mtindo wa
maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania, leo imeingia ubia na mgahawa ya Samaki Samaki ambao ilianzishwa tangu mwaka 2007
ukiwa na matawi matatu yaliyopo
Mlimani City, City Centre na Masaki Jijini Dar es salaam, ambapo pande hizo mbili zimekubaliana kufanya
kazi pamoja kwa kuleta bidhaa/huduma zao kwa wateja wa kila mmoja.
Akitangaza ubia huyo jijini Dar es
salaam leo, Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo Oliver Prentout aliviambia
vyombo vya habari kuwa ushirikiano huo
ni moja ya alama ambazo zinajenga imani
kwamba wateja wa Tigo ambao sasa wanaweza kujitambulisha kupitia migahawa ya Samaki Samaki
Tigo imeweka mtandao wa 4G LTE kwenye migahawa yote ya
Samaki Samaki ili kuwawezesha wateja
wake kufurahia intaneti ya kasi
na ya haraka wakati wakila na kunywa kwenye migahawa hiyo inayouza vyakula vinavyotokana na mazao ya baharini hapa
nchini.
“Tunaamini ushirikiano wetu utandelea kuonesha ni jinsi gani
tumejikita kwenye kuboresha mabadiliko kwenye mtindo wa maisha ya
kidijitali na kuongoza kwenye kutoa
teknolojia ya kisasa na ubunifu
kwa wateja wetu, alisema Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez.
Aidha Muasisi na Mkurugenzi wa migahawa ya
Samaki Samaki, Bw. Carlos Bastos alisema
Samaki Samaki wanawafanyia kazi Watanzania na wameungana na Tigo ambayo ni kampuni ya simu inayooongoza kwa
ubunifu nchini kuwapatia wateja
wake kile ambacho wamekisubiri kwa muda
mrefu kwa jinsi huduma za Tigo
zilivyo hususani uzoefu kwenye
mtandao wa bure na wa kasi wa intaneti.
Kwa ushirikiano huu tutawapatia wateja
wetu miradi mingi mipya, maboresho pamoja na ofa.
Kufanya kazi na Tigo sio kwamba
kunahusu sisi kupata fedha tu, bali
inahusu ni nini cha ziada tunachoweza
kuwapatia wateja wetu na hali kadhalika
ni kwa kiasi gani tunaweza kujifunza
kufanya kazi pamoja na kampuni
iliyo na uzoefu mkubwa na ya kimataifa.
Tunaweza kuwa ni mgahawa unaoongoza kwa vyakula vinavyotokan na mzao ya baharini, lakini tunapenda kufanya jambo zaidi kwa ajili ya wateja wetu.
Huduma za Tigo zinazotarajiwa
kuwepo kwenye migahawa ya Samaki Samaki
ni pamoja huduma ya bure ya
intaneti bila nyaya (WiFi), Tigo Pesa na
Tigo Music.
Post a Comment