Serikali yapongeza Uanzishwaji wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni TANZANIA
Serikali
yaipongeza Kampuni ya Quality Group ltd kwa hatua yake ya kuanzia Kituo cha
Uridhi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) ambapo kupitia kituo hicho bidhaa
mbalimbali za Sanaa na Utamaduni zinauzwa ndani na nje ya nchi.
Akitoa pongezi
hizo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema kuwa kuanzishwa kwa kituo
hicho kutaiuza nchi, utamaduni wetu, kazi za sanaa na kuongeza ajira miongoni
mwa jamii yetu.
Aidha Profesa
Gabriel amesema kuwa Serikali itaendelea kuwa pamoja nao na kushirikiana na
wadau wote ili kuhakikisha kwamba wanafikia mafanikio na malengo waliyojiwekea
katika uwekezaji huo.
Aliongeza kuwa
ni vyema sasa Kituo hiko kikafikiria kuanzisha vituo vidogo vidogo katika kanda
ili kurahishisha upatikanaji wa bidhaa hizo na kusaidi wasanii walioko
pembezoni wapate soko la bidhaa zao kwa Serikali ingependa kuona zaidi wasanii
wa ndani wakinufaika na uwepo wa Kituo hicho.
..................
Kwa upande wake
Afisa Mtendaji Mkuu wa Quality Group Limited Bw. Arif Sheikh ameishukuru
Serikali kwa kuonyesha ushirikiano kna imekuwa faraja kubwa kwao kwa kiongozi
wa ngazi ya juu Serikalini kukubali kuja kuzindua Kituo chao.
Sheikh amesema
kuwa kuanzishwa kwa Kituo hicho kumelenga kukuza sanaa na utamaduni wa
Mtanzania kwakuwa kinahusika na uuzaji wa bidhaa za sanaa na utamaduni tu,
hivyo wasanii wanayo fursa ya kujipatia kipato kwa kukiuzia Kituo kazi zao.
Hata hivyo
Sheikh alisema kuwa kutokana na ushauri uliotolewa Kampuni yao ipo tayari kutoa
ushirikiano zaidi kwa Serikali pindi watakapohitajika kufanya hivyo ikiwemoi
sualaua la kuwajengea uwezo wasanii wa kazi za mikono.
Kituo cha Urithi
wa Utamaduni Tanzaia ambacho kwa kingereza kinaitwaTanzania Center for Cutural Heritage (TCCH)kipo katika jengo la
Quality Center, kinamilikiwa na Kampuni ya Qaulity Group Limited ya jijini Dar
es Salaam.
Post a Comment