Waziri UMMY MWALIMU ataka Ripoti ya Kuwakopesha Wanawake
Na Catherine Sungura,Msalala
Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala wilayani kahama,amepewa wiki mbili awe amempatia ripoti waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto, Ummy Mwalimu ,wanawake wanaoponda kokoto wamewezeshwaa kwa kupatiwa mkopo wa kiasi gani na mafunzo yapi.
Hali hiyo imetokea wakati waziri huyo alipofika halmashauri hiyo kukagua ujenzi wa kituo cha afya kilichopo kata ya bugarama kinachojengwa na kampuni ya mgodi wa ACACIA iliopo Bulyahulu na kuwakuta wanawake mbele ya majengo hayo wakiponda kokoto kwa kutumia vifaa duni na vya mkono
Waziri Ummy alisema hivi sasa kuna vitendea kazi vya Kisasa na vya bei rahisi ambayo vitawasaidia wanawake hao kuwarahisishia wanawake kuacha kushinda masaa kumi wakiponda mawe
"Baada ya makusanyo ya Mapato ya ndani,mkurugenzi unatakiwa kutenga asilimia 5 kwa ajili ya vikundi vya akina mama na sio vikundi vya kujitafutiza huko mitaani na vya kujuana"
Waziri Ummy alisema haiwezekani wanawake wanaojishughulisha na shughuli ndogondogo wakaachwa pasipo kusaidiwa kwani wanawake wengi ndio wanaosaidia familia.
"Tusipowawezesha wanawake hawa,mnataka tuwawezeshe wanawake gani?hawa ndio waliotupigia kura hawa,lazima tuwaonyeshe maneno ya Rais Magufuli hayakuwa matupu mana alisema anataka kuwawezesha wanawake na ndo mana kila halmashauri inatakiwa kutenda asilimia kumi ya mapato yake kwa ajili hii"
Aidha,alisema wawahamasishe wanawake wengine katika Kata zote kujiunga kwenye vikundi hususan wale wanaojituma na kujitoa kwa biashara ndogondogo
wanawake hao wapatao thelathini wanaoponda kokoto karibu na kituo cha afya Bugarama walisema wanaomba wanawake wawezeshwe kwani hawajui kama kuna pesa zinatakiwa kutengwa kwa ajili ya wanawake,hata hivyo walimshukuru waziri huyo kwa kuwafumbua macho.
Naye mganga mkuu wa halmashauri hiyo dkt. Hamad Nyembea alisema kampuni hiyo ya ACACIA ilianza ujenzi wa kituo cha afya julai,2014 na hadi kukamilika ujenzi huo itagharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.7, na ujenzi wa zahanati ya bulyahulu itagharimu zaidi ya milioni mia tatu
Waziri Ummy Mwalimu Ataka Ripoti Ya Kuwakopesha Wanawake - Habari 360 >>>>> Download Now
ReplyDelete>>>>> Download Full
Waziri Ummy Mwalimu Ataka Ripoti Ya Kuwakopesha Wanawake - Habari 360 >>>>> Download LINK
>>>>> Download Now
Waziri Ummy Mwalimu Ataka Ripoti Ya Kuwakopesha Wanawake - Habari 360 >>>>> Download Full
>>>>> Download LINK Od