TWIGA STARS yaelekea Visiwani ZANZIBAR
Timu ya Twiga Stars ikiondoka kwenda Zanzibar kwa ajili ya kambi ya mazoezi.
Wachezaji wa Tiga Stars wakiwa Feri wakisubiri boti ya kwenda Zanzibar kwa ajili ya kupiga kambi ya mazoezi.
……………………………………………………………………
Kikosi cha timu ya Timu ya Taifa
ya Wanawake (Twiga Stars) kimeodoka leo saa 6 mchana jijini Dar es
salaam kuelekea kisiwani Zanzibari, ambapo kitaweka kambi ya mwezi mmoja
kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) mwezi
Septemba.
Msafara wa Twiga Stars umeondoka
na boti ya Azam (Kilimanjaro) ukiwa na watu 32, wakiwemo wachezaji 25,
benchi la ufundi 6 pamoja na kiongozi wa msafara, ambapo TFF imegharamia
kambi hiyo ya mwezi mmoja.
Wachezaji waliosafiri leo ni
Fatuma Omari, Belina Julius, Happiness Hezron, Fatuma Hassan, Anastazia
Anthony, Fatuma Bashiru, Fatuma Issa, Fatuma Khatibu, Maimuna Hamis,
Donizia Daniel, Sofia Mwasikili, Etoe Mlenzi.
Wenigine ni Amina Ally, Thereza
Yonna, Mwanahamisi Omari, Stumai Abdallah, Shelder Boniface, Asha
Rashid, Najiat Abbas, Estha Chabruma, Mwajuma Abdallah na Fatuma
Mustapah.
Twiga Stars itakua kambini
kisiwani Zanzibar kwa kipindi cha mwezi mmoja, kujiandaa na fainali hizo
za michezo ya afrika, ambapo imepangwa kundi A pamoja na wenyeji Congo –
Brazzavile, Ivory Coast na Nigeria.
Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) zinatarajiwa kuanza kutivua vumbi Septemba 4 – 19 nchini Congo-Brazzavile.
Post a Comment