Mwanaharakati Aliyechungulia Kifo ameondoka BURUNDI
Mwanaharakati maarufu wa haki za
kibinaadamu nchini Burundi aliyepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na
watu waliokuwa katika pikipiki anaondoka nchini humo kuelekea nchini
Ubeljiji.
Amekuwa mkosoaji mkubwa wa tangazo la rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu,hadi kufikia sasa haijajulikana ni nani aliyekuwa amelenga kumtoa uhai.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon alikuwa miongoni mwa viongozi wa kimataifa waliotaka uchunguzi wa kina ufanyike ilikubaini nani aliyemshambulia bwana Mbonimpa.
Shambulizi hilo lilifuatia lile la jumapili wiki iliyopita ambapo mshauri wa rais Nkurunziza, jenerali Adolphe Nshimirimana aliuawa katika shambulizi ndani ya gari lake mjini Bujumbura.
Burundi imekabiliwa na ghasia tangu hatua ya rais Nkurunziza mnamo mwezi Aprili kutaka kuwania muhula wa tatu.
Wapinzani wamedai kwamba hatua hiyo ni kinyume na katiba huku jaribio la mapinduzi likifeli mnamo mwezi Mei.
Uchaguzi wa urais ulifanyika mwezi uliopita ambapo bwana Nkurunziza alishinda lakini ulisusiwa na upinzani.



Post a Comment