Header Ads

Mgombea Nafasi ya Urais Kupitia Chadema, EDWARD LOWASSA alipowasili na Kuzungumza na Wananchi Jijini Mbeya

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa akiwapumbia maelfu ya wakazi wa Jiji la Mbeya, waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Ilomba leo Agosti 14, 2015. Mh. Lowassa na Mgombea mwenza wake Dkt. Juma Haji Duni, walikuwa jijini humo kwa ajili ya zoezi la kutambulishwa kwa wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu" akimueleza jambo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa, wakati akiwahutubia wananchi wa Jiji la Mbeya.

Umati wa wananchi wa Jiji la Mbeya ukiwa umefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Ilomba Kwa ajili ya kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia Chadema Edward Lowassa leo Agosti 14, 2015.

No comments

Powered by Blogger.