Header Ads

Bodi ya Mikopo Yaahidi Kutekeleza Majukumu yake


Na Jenikisa Ndile-Maelezo

Idadi ya wanafunzi wanaopata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imekuwa imeongezeka mwaka hadi mwaka na kusaidia kuongeza idadi ya watanzania wanaopata elimu ya juu. Katika mwaka wa masomo wa 2005/2006 Bodi ya Mikopo ilitoa mikopo kwa wanafunzi 42,729 iliyogharimu sh. bilioni 56.1 na mwaka wa masomo wa 2014/2015 bodi ya mikopo ilitoa mikopo kwa wanafunzi 98,000 iliyogharimu shilingi bilioni 345. 

 Hayo yalisemawa leo na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka bodi hiyo Cosmas Mwaisobwa wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (MAELEZO) kuhusu mafanikio ya bodi hiyo katika kipindi hicho. Alisema kwa kipindi hicho chote wamekuwa na sheria mbalimbali ilioanzishwa kwa kuwapa jukumu la ukusanyaji wa madeni ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ambayo ilianza kutolewa tangu mwaka 1994/1995 kupitia iliyokuwa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia wakati huo Serikali haikukusanya madeni kutoka kwa wanufaika hadi pale bodi ilipoanza kazi rasmi mwaka 2006/2007. 

 Aliongeza kuwa taasisi hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kulinganisha na hapo awali kwani kwa kipindi cha miaka kumi tumeongeza ufanisi katika matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kwa lengo la kuomba mikopo kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa uombaji wa mikopo wa (OLAMS) Aidha bodi hiyo imeendelea kukua kwa kasi kutokana na idadi ya watumishi kutoka tisa hadi kufikia watumishi 135 mwaka huu,ongezeko hilo limesaidia bodi kuwa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake. 

 Bodi hiyo imewawezesha wateja wake kupata huduma katika maeneo manne ambayo ni Arusha, Mwanza, Dodoma, na Zanzibar ili kupata huduma za kibodi kwa ukaribu zaidi. Mwaisongwa aliwahakikishia wateja hao wataendelea kuwanufaisha waombaji na kutambua kuwa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya uchangiaji wa elimu ya juu na ni muhimu kurejesha mikopo ili kuwezesha mfuko huo kuwa endelevu. 

Taasisi hiyo iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria namba 9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi julai 2005 yenye lengo la kutoa mikopo kwa wanafunzi i wa elimu ya juu,utoaji na ukusanyaji wa mikopo ili kufanya mfuko wa mikopo kuwa endelevu.

No comments

Powered by Blogger.