Waziri UMMY MWALIMU azindua Duka la Dawa la MSD Kanda ya Mbeya
Na Rabi Hume
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amefanya uzinduzi wa duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa Kanda ya Mbeya.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mwalimu amesema uzinduzi wa duka hilo ni sehemu ya jitihada zinazofanywa na serikali ya Rais Magufuli kuwatia wananchi huduma bora na kwa gharama nafuu.
“Neema hii imekuja kwa kipindi cha Rais Magufuli, sasa amekidhi matakwa na shauku ya wananchi wa Mbeya kwa kuwapa duka la dawa,
“Sera ya huduma ya afya inataka wananchi wachangie isipokuwa wazee, watoto na wajawazito na kupitia duka hili wananchi wataweza kupata dawa kwa gharama nafuu,” amesema Mhe. Mwalimu.
Duka hilo la dawa la Kanda ya Mbeya limetumia Shilingi Milioni 13 kwa ukarabati wa jingo na vifaa vyake.
Mh.Ummy Mwalimu akionesha moja ya dawa inayouzwa dukani hapo kwa shilingi 7,000 ambapo kwenye maduka binafsi inauzwa shilingi 25,000,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurine Bwanakunu na kulia ni Mfamasia wa duka hilo, Cornel Mkeng'e.
Mfamasia wa Duka la Dawa, Cornel Mkeng'e akitoa maelezo kwa Mh.Ummy Mwalimu mara baada ya kuzindua duka hilo.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiangalia jinsi ya ufungashaji wa dawa kwenye ghala jipya la Kanda ya Mbeya.ghala hilo limelozinduliwa leo jijini Mbeya.
Duka la Dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Kanda ya Mbeya ambalo litahudumia mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akipata maelezo jinsi ya utunzaji dawa kwenye ghala hilo.
Post a Comment