Header Ads

Waziri UMMY MWALIMU akagua Hospitali ya MBEYA


Na Catherine Sungura

Hospitali zinazotumia mfumo.wa ukusanyaji mapato wa  kielectronik wametakiwa wasibweteke na mapato wanayoyakusanya kila siku.

Rai hiyo.imetolewa na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mh.Ummy Mwalimu wakati alipotembelea hospitali ya rufaa ya kanda ya mjini Mbeya

Ummy alisema ukusanyaji wa mapato kwa mfumo huu unasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha huduma za afya nchini ikiwemo ununuzi wa dawa,vifaa na vifaa tiba pamoja na utoaji wa motisha kwa watumishi
"Bado tunatambua hali ya uhaba wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kuanzia ngazi zote,tukiweza kusimamia vizuri hili tutafanikiwa"alisema

Aidha alisema wanatarajia katika serikali ya awamu hii bajeti ya dawa itaongezeka zaidi ya mara tatu kulinganisha na bajeti za nyuma,hivyo wameishauri bohari kuu ya dawa wanunue dawa toka kwa wawekezaji wa hapa nchini ambapo itakua na bei nafuu na itaongeza tija na upatikanaji wa dawa kwa haraka

waziri Ummy Mwalimu aliutaka Mkoa kufuatilia,kuwafichua na kuwachukulia hatua wale wote watakaojihusisha na wizi wa dawa

"Tunao watumishi wachache wa afya ambao wanahujumu na kuiba dawa na kuzipeleka kwenye maduka ya.dawa binafsi,hao hatutowafumbia macho na kuwapeleka mahakamani"

Kuhusu upungufu wa watumishi wa kada ya afya nchini ,Wazirini wa afya alisema,nchi ina upungufu wa asilimia 52,hivyo.serikali inatarajia kuajiri watumishi takribani elfu kumi hivi karibuni ambao watatawanywa nchi nzima ikiwemo mikoa iliyo pembezoni

Katika hospitali ya uzazi ya Meta,waziri huyo ameguswa na ufinyu wa wodi za wazazi na kupelekea mama wajawazito na waliojifungua kulala chini na wawili wawili kwenye kitanda kimoja na hivyo kuwataka kufanya haraka ujenzi wa jengo jipya litakaloondoa mrundikano wa mama wajawazito na watoto njiti

Hospitali ya kanda ya rufaa Mbeya inakusanya kwa mwezi kiasi cha shilingi mia tano,inahudumia mikoa saba nchini na kuhudumia zaidi ya watu milioni mbili.

No comments

Powered by Blogger.