Na Mwandishi Maalumu
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mh. Luhaga Mpina, amewataka watendaji katika ngazi za uteuzi nchini
kushiriki kikamilifu katika kuhahikisha usalama wa rasilimali za misitu.
Naibu Waziri Mpina ameyasema hayo leo katika Pori la Ruvu
Kaskazini ikiwa ni siku ya Kitaifa ya kupanda miti na kueleza kuwa Serikali
imekuwa na lengo la kupanda miti milioni moja nukta tano (milioni 1.5) kwa
mwaka mzima katika kila wilaya, na kuwataka watendaji waliopo katika ngazi za
uteuzi yaani Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu wakuu,
kuhakikisha lengo hili linafikiwa na kueleza kuwa viongozi watakaoshindwa kusimamia zoezi hili
majina yao yatapelekwa katika mamlaka za uteuzi na kuchukuliwa hatua, hii ikiwa
ni njia ya kupima usalama wa rasilimali hizi.
Akiongea na wananchi katika Pori la Ruvu Kaskazini, Mh. Mpina
alisema kuwa asilimia 61 ya ardhi ya nchi ipo kwenye hatari ya kuwa jangwa
kutokana na uharibifu wa mazingira
utokanao na ukataji miti ovyo, na
takwimu zinaonyesha kuwa takribani hekta laki tatu nukta sabini na mbili
za misitu zinakatwa kila mwaka kwa matumizi mbali mbali. “mikoa nane nchini iko
hatarini kuwa jangwa”. Alisisitiza.
|
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mh. Luhaga Mpina akipanda Miti
katika Hifadhi ya Msitu wa ruvu kaskazin
uliyopo kibaha Mkoani Pwani mapema hii leo,wengine ni Baadhi ya wakurugenzi
wakishuhudia Upandaji huo.
.................................
Akielezea athari, zitokanazo na uharibifu wa misitu, Mh. Mpina alisema taifa
linaweza kutumia mabilioni ya fedha kwa ajili ya kununua chakula kuwalisha wa
Tanzania kutokana na ukosekanaji wa mvua ,vyanzo vya maji kukauka, upatakinaji
wa umeme kuwa wa kusuasua kutokana na uharibifu wa misitu na vyanzo vya maji.
Kwa upande Mwingine Mh. Mpina alisema kuwa serikali imekata
miti kwa sababu mbalimbali za msingi ikiwa ni pamoja ujenzi wa miundo mbinu
kama vile barabara, reli ujenzi wa bomba la gesi, hivyo basi kuna jukumu kubwa
la kupanda miti mingi zaidi ya hiyo iliyokatwa.
Akitolea Mfano wa taasisi za huduma ya misitu Nchini (TFS)
iliyopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii,
Mh. Mpina aliainisha kuwa taasisi zote za serikali zisaidie taifa
kubainisha ni mazao gani ya misitu
yanaweza kupandwa katika maeneo gani kulingana na mahitaji ili kuweza kunusuru
upotevu wa rasimali ya misitu.
|
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Mh.Luhaga Mpina akitoa maelekezo kwa Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Injinia Angelina Madete(
katikati) kuhusu upandaji miti katika sehemu mbalimbali katika hifadhi ya
misitu kibaha Mkoani Pwani,mapema hii leo katika siku ya upandaji miti.
( Kwa Hisani ya EVELYN MKOKOI )
|
Post a Comment