Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri waagizwa Kuzingatia Mikataba ya Kazi na Ajira kwa Madereva
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama (Mb) ameiagiza kamati ya Kudumu ya Waziri Mkuu ya Kutatua
kero na changamoto katika sekta ya usafiri wa barabara kuangalia upya mikataba
ya madereva ili kuhakikisha haki za madereva zinalindwa.
Mhe mhagama alitoa agizo hilo wakati wa mkutano wake na Kamati hiyo uliofanyika Aprili 1, 2016 katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuangalia namna bora ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya usafirishaji.
Katika kikao cha Kamati hiyo inayoundwa na Wamiliki wa malori, daladala, mabasi, vyama vya abiria, Idara ya Usafirishaji, Shirika la viwango, Wakala wa Vipimo, Jeshi la polisi, watu wa usalama barabarani, TANROADS na Umoja wa Wasafirishaji Abiria Dar es Salaam (UWADAR) mhe. Mhagama alisisitiza kuwa Serikali haitawafumbia macho wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao hawazingatii mikataba ya kazi kwa madereva.

Post a Comment