Na Mwandishi
Wetu,
Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kushirikiana na Mfuko wa Kusaidia
Kilimo (PASS) wameingia makubaliano ya kudhamini mikopo kwa wakulima wasio na
dhamana watakaokopa kupitia TADB.
Wakizungumza
katika hafla ya kuwekeana saini makubaliano hayo, yaliyofanyika katika Ofisi za
TADB, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi
na Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay wamesema kuwa katika kukabiliana
na changamoto za ukosefu wa dhamana za uhakika, kunakochagiza ukosefu wa upatikanaji
wa mikopo kwa wakulima taasisi hizo zimekubaliana kuwawekea dhamana wakulima
wenye sifa ya kukopesheka katika Benki hiyo ila wanakosa dhamana waweze
kudhaminiwa na PASS.
|
Post a Comment