Na Mwandishi Maalumu
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga Bi. Anne Kilango Malecela
na Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul Rashid Dachi, kufuatia mkoa huo kutoa
taarifa zisizo sahihi kuwa hauna watumishi hewa.
Rais Magufuli
ametangaza kutengua uteuzi wa Viongozi hao wa Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 11
Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, mara baada ya kupokea Taarifa ya Mwaka
2014/2015 ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), na kupokea
hundi kifani ya shilingi Bilioni 6 kutoka Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania zilizotokana na kubana matumizi.
Dkt. Magufuli
ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa kuwa Mkoa wa Shinyanga hauna watumishi
hewa, aliamua kutuma timu ya ukaguzi iliyokwenda kufanya uchunguzi ambapo hadi
kufikia jana tarehe 10 Aprili, 2016 imebaini kuwepo watumishi hewa 45 huku
zoezi likiwa linaendelea katika wilaya mbili za Ushetu na Shinyanga Vijijini.
|
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Mwaka ya utendaji wa Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo
Kamishna Valentino Mlowola Ikulu jijini Dar es Salaam.
|
|
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hundi Kifani yenye thamani ya Shilingi
Bilioni Sita kutoka kwa Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson mara baada ya Taasisi ya Bunge
kutekeleza kwa vitendo kauli ya kubana matumizi yasio na Tija ili fedha hizo
zikanunulie madawati kwa ajili ya wanafunzi.
|
|
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameishika Taarifa ya Mwaka ya utendaji wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mara baada ya kukabidhiwa
na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna Valentino Mlowola Ikulu jijini Dar
es Salaam. |
|
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kabla ya kukabidhiwa
hundi kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita.
|
|
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika tukio hilo la upokeaji wa Taarifa
yaUtendaji wa TAKUKURU pamoja na
upokeaji wa Hundi Kifani kutoka Taasisi ya Bunge Ikulu jijini Dar es Salaam.
|
|
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo katika Hotuba yake ambayo pia
alitengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ane Kilango Malecela ambaye
alikubali kutoa taarifa ambazo si sahihi kuwa Mkoa wa Shinyanga hauna watumishi
hewa, japo katika uhakiki uliofanyika mara baada ya taarifa hiyo kumebainika
kuwa kuna zaidi ya watumishi 45 ambao ni hewa.
"Na wale wote
wa Shinyanga ambao walisemekana ni zero, hakuna mtumishi hewa, walikuwa tayari
wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza sana, na nikajiuliza sana na
kwa kweli nimejiuliza sana na kwa masikitiko makubwa, kwa nini Mkuu wa Mkoa
alisema hakuna mtumishi hewa?" Amesisitiza Rais
Magufuli
Rais Magufuli amesema
baada ya kutengua uteuzi wake, Anne Kilango Malecela atapangiwa kazi nyingine.
Pamoja na hatua
hiyo, Dkt. Magufuli ametaka wakuu wa mikoa yote wawafichue watumishi hewa wote
ili waondolewe mara moja, na ameagiza timu iliyofanya uchunguzi Mkoani
Shinyanga itumike kufanya uchunguzi katika mikoa mingine kwa lengo la kukomesha
upotevu mkubwa wa fedha za umma.
Katikati ya Mwezi
Machi, 2016 Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa yote nchini kusimamia zoezi
la kuwaondoa watumishi hewa wote katika orodha ya malipo ya mshahara, ambapo
mpaka tarehe 31 Machi, 2016 Jumla watumishi hewa 5,507 walibanika.
Kati ya shilingi
Bilioni 583 ambazo serikali imekuwa ikitumia kila mwezi kwa ajili kulipa
mishahara, kati ya shilingi Bilioni 53 na 54 zimekuwa zikipotea kutokana na
kulipa mishahara ya watumishi hewa.
|
|
Baadhi
ya Viongozi wa juu wa Jeshi la Magereza pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa JKT
wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli aliyokuwa akiyatoa Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
|
Post a Comment