Rais Dkt JOHN MAGUFULI akabidhi Shilingi Milioni 10 Kusaidia Upanuzi wa Kanisa Wilayani CHATO
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Sakramenti takatifu kutoka kwa Paroko wa Parokia
ya Bikira Maria Chato Padre Henry Mulinganisa.
|
Na Mwandishi Maalumu
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa Mchango wa Shilingi
Milioni 10 kwa Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita kwa ajili
kuchagia upanuzi wa kanisa hilo.
Fedha hizo
zimekabidhiwa na Kaimu Mnikulu Bw. Ngusa Samike katika misa ya pili ya ibada ya
Jumapili ya pili ya Pasaka, iliyofanyika kanisani hapo leo tarehe 03 April,
2016.
Kabla ya misa hiyo
ya pili Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa pamoja na Waziri
Mkuu Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Amoro Odinga na Mkewe Mama Ida Odinga,
walisali misa ya kwanza ambapo Rais Magufuli aliahidi kuchangia shilingi
milioni 10 kwa ajili ya upanuzi wa kanisa hilo ambao unaendelea.
Katika Misa hiyo
Paroko wa Parokia ya Chato, Padre Henry Mulinganisa alieleza kuwa kanisa hilo
linatarajia kuadhimisha miaka 50 ya tangu kuanzishwa kwake baadaye mwaka huu,
na kwamba maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na upanuzi wa kanisa ambao
unachangiwa na waumini wenyewe.
Padre Mulinganisa
amemshukuru Rais Magufuli kwa mchango huo, na amemuahidi kuwa utatumika vizuri
ili uendeleze upanuzi wa kanisa hilo pamoja na michango ya waumini wengine.
Post a Comment