Naibu Waziri wa Afya Dkt HAMIS KIGWANGALLA atembelea Hospitali ya Mkoa wa Manyara
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Hospitali ya Mkoa wa Manyara pamoja na Kituo cha Afya Magugu kilichopo Wilayani Babati ambapo ametoa maagizo mbalimbali ya kiutendaji na sera katika utoaji wa huduma kwenye sekta ya Afya nchini.
Dkt. Kigwangalla alianzia katika Hospitali ya Mkoa wa Manyara na kisha kuagiza uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Manyara kuwa na chumba maalumu cha kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum ((ICU) angalau kuwa na vitanda viwili vya kuanzia.
Dkt. Kigwangalla alibaini changamoto mbalimbali licha ya kuwa na majengo machache na mapya, katika Hospitali hiyo inakabiriwa na ukosefu wa chumba cha wagonjwa hao mahututi hivyo kuagiza Katibu Tawala na Mganga Mkuu wa Mkoa, Bw. Eliakim Maswi kuhakikisha wanaanza na vitanda viwili hadi vitatu vinapatikana haraka ilikuwa na uwezo wa kusaidia wagonjwa wanaofikishwa hapo ilikupatiwa uangalizi maalum.
Dkt. Kigwangalla amebainisha kuwa, Hospitali kubwa kama hiyo kukosa chumba cha ICU ni hatari endapo itatokea tatizo kubwa hivyo kuagiza kulichukulia hatua za haraka.
Aidha, Naibu Waziri amesikitishwa na hali aliyokutana nayo kwenye maabara ya Hospitaali hiyo kutokuwa na damu za kutosha kwenye benki yake na kumuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Ally Uledi, kuanisha mipango ya upatikani wa damu salama katika kipindi cha siku 30.
Katika benki hiyo ya damu, Dkt. Kigwangalla aliweza kushuhudia kukiwa na damu unit 3 badala ya 150 zinazohitajika.
Aidha, Dkt. Kigwangalla alifunga safari hadi Wilaya ya Babati na kukagua kituo cha Afya Magugu na kukagua mambo mbalimbali katika kituo hicho huku akitoa maagizo ya kiutendaji huku akitaka apatiwe taarifa ambazo wanahitaji kusaidiwa zile zinazoihusu Wizara yake ilikushughulikiwa haraka.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akiwasili katika Hospitali ya Mkoa wa Manyara.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo namna ya kitengo cha maabara ya Hospitali ya Mkoa wa Manyara inavyofanya kazi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa maelezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Bw. Eliakim Maswi juu ya kufanyia marekebisho vifaa vya Maabara.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt.Hamisi Andrea Kigwangalla akiangaliaa benki ya damu ambayo haina kabisa damu licha ya kutolewa miongozo ya kila Hospitali kuwa na benki yake ya damu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla (katikati) akipatiwa maelezo ya kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Manyara. Kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Ally Uledi.
..Ziara ikiendelea
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa maelezo namna ya ramani ya chumba cha upasuaji kinavyotakiwa kujengwa.
Chumba cha kutakasia vifaa maalum vya upasuaji.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitafakari jambo wakati alipokagua chumba cha upasuaji.
..Wakisikiliza maswali ya watendaji wa Hospitali.
Baadhi ya viongozi na madaktari wa Hospitaali ya Mkoa wa Manyara wakifuatilia mkutano huo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa maelezo kwa uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Manyara..
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Bw. Eliakim Maswi akifafanua jambo katika mkutano huo.
Post a Comment