Mkurugenzi wa Mji KAHAMA apewa Siku 90 Kununua Mashine ya Mionzi
Na Catherine Sungura,kahama
Mkurugenzi wa halmashauri wa mji kahama amepewa siku tisini awe amenunua mashine ya mionzi (x ray)kwa ajili ya hospitali ya mji kahama.
Agizo hilo amepewa jana na Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy mwalimu wakati alipotembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa kada ya afya wa wmji huo.
Waziri Ummy alisema ametoa agizo hili ili kuweza kurahisisha usumbufu wanaupata wananchi wa wilaya hiyo kwa kwenda kupata huduma nje ya hospitali ambapo wakati mwingine vipimo hivyo vinakuwa havisomeki vizuri kwa kukosa viwango vinavyostahili za mashine hizo.
Hata hivyo waziri ummy alisema upatikanaji wa mashine hizo itapunguza malalamiko mengi toka kwa wananchi kwa ukosefu wa kifaa tiba hicho ili kwani hospitali hiyo hivi sasa inahudumia wananchi zaidi ya milioni moja hususan toka wilaya zote za wilaya hii.
Aidha, alizitaka halmashauri zote mjini kuweza kuwekeza kwenye huduma za vifaa tiba ambavyo inarahisisha kugundua matatizo yanayowakabili wananchi wanaofika kwenye kupata huduma na hivyo kuwapatia matibabu stahili wagonjwa wanaofika kupata matibabu kwenye vituo vya kutolea huduma nchini.
“siku hizi lazima muwekeze kwenye kununua vifaa tiba ili kuweza kupata kutoa huduma nzuri ,pesa mnakusanya na kahama ni halmashauri tajiri,mkurugenzi nakupa siku tisini uwe umenunua mashine hiyo.
Naye mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Vita kawawa amemuahidi waziri huyo kwamba amepokea maagizo yote aliyoyatoa na atayafuatilia ili kuweza kutatua malalamiko ya wananchi na yale ya watumishi wa kada ya afya.
Post a Comment