Kamati ya Kudumu ya Bunge ya KILIMO, MIFUGO na MAJI yaridhishwa na Matumzi ya Fedha Mtambo wa Ruvu Chini
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imeridhishwa na
matumizi ya fedha kiasi cha shilingi Bilioni 141 zilizotolewa na
Serikali kugharamia mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la maji kutoka
Mtambo wa Ruvu Chini,wilayani Bagamoyo kwenda jijini Dar es salaam
kufuatia ujenzi wake kukamilika.
Akizungumza mara baada ya Kamati hiyo kutembelea maeneo mbalimbali ya
mradi huo ikiwemo mtambo wa Maji wa Ruvu Chini ulioko Bagamoyo mkoani
Pwani, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Hanan'g Mhe. Mary Nagu amesema kuwa kamati kamati yake imeridhishwa
na ubora wa kazi iliyofanyika chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Maji
Safi na Maji Taka Dar es salam ( DAWASA).
Amesema mradi huo wenye urefu wa kilometa 56 umekamilika na kueleza
kuwa itakua historia kwa wananchi wa Dar es salaam waliounganishwa
na mtandao wa mabomba ya DAWASCO kukosa maji.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakiangalia mitambo ya kuchujia maji kutoka mto Ruvu kwenye Mtambo wa maji wa Ruvu Chini. |
Sehemu ya kuchujia maji katika mtambo wa Ruvu Chini. |
Post a Comment