Mama wa Shujaa wa Chakula yawapeleka Watatu Nje ya Nchi
Mshindi
wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2014 Linaloendeshwa na Oxfam
kupitia kampeni yake ya Grow Bahati Muriga(Kulia) yenye kauli mbiu
kuwa Wekeza kwa wakulima wadogo wanawake Inalipa, akielezea kwa undani
juu ya Safari yake ya Kwenda Marekani pia Kushukuru Oxfam kwa kupata
nafasi hiyo.
Aliyekuwa
Mshiriki wa Shidano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa nne 2015 Eva
Mogeni (Kushoto) akielezea kuhusu safari yao ya kwenda Addis Ababa
Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa
African Rural Woman Assembly (ARWAA) na kutunga Sera juu ya kilimo na kupaza sauti za wakulima wadogo hasa wanawake ili kupata Fursa sawa katika Kilimo.
Edna Kiogwe aliyekuwa Mshiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 akielezea jambo kuhusiana na kuhudhuria mkutano wa
African Rural Woman Assembly (ARWAA) utakaofanyika Adis Ababa nchini Ethiophia
Oktoba 11hadi 15 mwaka huu.
Waliokuwa washiriki wa
Shindano la Mama Shujaa wa Chakula akiwemo Mshindi wa Shindano hilo kwa Mwaka
2014 Msimu wa tatu Bahati Muriga Wamepokea Mwaliko wa Kwenda Washington DC
Marekani kuhudhuria mkutano mkuu wa Siku ya Chakula duniani unaotarajiwa
kufanyika Washington DC na Addis Ababa
kwa ajili ya Kuhudhuria Mikutano Mbalimbali. Kati ya hao Bahati Muriga
atakwenda Marekani na Edina Kiogwe
pamoja na Eva Mogeniw watakwenda kuhudhuria
mkutano wa African Rural Woman Assembly (ARWAA).
.............................................
.............................................
Eluka Kibona ambaye ni
Meneja wa Utetezi wa Oxfam Tanzania alisema kuwa Bahati Muliga atahudhuria
mikutano mbalimbali nchini humo inayohusu masuala ya Chakula na Kilimo wakati
wa wiki zote Mbili atakazokuwa huko. Aliongeza kuwa Oxfam imethibitisha kupokea
Barua ya Mwaliko wa Muriga na atahudhulia kikamilifu makongamano hayo ili apate
kujifunza na kupata ujuzi ambao atautumia kwa kuwashirikisha wakulima wanawake
wadogo wadogo.
“Muriga anakwenda kuhudhuria mikutano mingi,
ambayo itafanyika Washington DC na Ohio. Hii ni fursa adimu ambayo Shirika la Oxfam
kupitia Oxfam Tanzania limeamua kutoa kwa kinamama hawa ili wajifunze zaidi
kilimo cha kisasa na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,” alisema
Eluka.
Wakati huo huo Oxfam
wakishirikiana na Shirika la Kimataifa la Action Aid na African Union
Commission limetoa Mwaliko kwa washiriki wawili kati ya walioshiriki shindano
la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa Nne ambao ni Edina Kiogwe na Eva Mogeni kuhudhuria mkutano
wa African Rural Woman Assembly (ARWAA) utakaofanyika Adis Ababa nchini
Ethiophia unaotarajiwa kuanza Tarehe 11 Octoba mwaka huu
Eluka alisema Mkutano huo
unawakutanisha na kuwaleta pamoja vikundi vya wazalishaji chakula wadogo kutoka
sehemu mbalimbali Afrika kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wao wanavyohusika na
watengeneza sera na kutoa mchango wa pamoja kukabiliana na mahitaji yao.
Akizungumzia safari hiyo
Mshindi wa Mama Shuja wa Chakula Msimu wa Tatu Bahati Muriga alisema hiyo ni
fursa mpya kwake na anajua kwa kuhudhuria mkutano huo atapata maoni mapya
kuhusiana na sera ya kilimo, uwekezaji katika miradi, lakini kubwa zaidi ni
kwake ni mbinu mbadala za kilimo cha kisasa sambamba na kushuhudia nini wengine
wanafanya katika kilimo.
“Nitapata maoni mapya ninakwenda kwa niaba ya
wakulima wadogowadogo Tanzania, lakini kuongeza ujuzi na kupata mikakati
mbalimbali kuhusu kilimo, kujuana na kubadilishana mawazo, kupata
mahusiano mapya na kujenga mikakati,” alisema Bahati Muriga.
Nae aliyekuwa Mshiriki wa
Shindano lala Mama Shujaa wa Chakula msimu wa nne Eva Mogeni akizungumzia Juu
ya Safari hiyo alisema hii ni Fursa kwa wakulima wadogo wadogo kupaza sauti zao
kuhusiana na kilimo, pia aliongeza Fursa hii aliyoipata kutoka Oxfam itakuwa ni
Chachu kwake kujifunza mambo mapya na yenyekuleta maendeleo zaidi.
Edina Kiogwe ambaye
alishiriki mashindano ya mwaka huu alisema anatarajia mafunzo atakayoyapata
yatamjenga na kumwongezea ujuzi zaidi, lakini pia aliwahamasisha wakulima
wanawake wadogowadogo kujituma na kujitoa katika mashindano mbalimbali ili
kupaza sauti zao na kupata fursa mbalimbali.
Post a Comment