UGANDA imepiga Marufuku Urejeshaji wa Mahari
Mahakama ya juu zaidi nchini Uganda
imesema kuwa utamaduni wa kurejesha mahari baadaya talaka katika ndoa za
kitamaduni unakiuka katiba na utamaduni huo unapaswa kupigwa marufuku.
Jaji mkuu wa Uganda Bart Magunda Katureebe amesema kuwa ikiwa utamaduni huo utaruhusiwa kuendelea itakuwa na maana kuwa wanawake ni kama bidhaa zinazouzwa sokoni.
![]() |
Ngombe hutumiwa sana kulipa mahari Uganda |
Hata hivyo mmoja wa majaji hao alisema kuwa utamaduni huo unawadhalilisha wanawake na kwamba mahakama inapaswa kulifanya swala la ulipaji mahari kuwa chaguo na wala sio sharti.
Post a Comment