Watanzania
hususan wale wanaosafiri nje ya nchi zile zenye ugonjwa wa homa ya manjano
wanatakiwa kujitokeza kwenye vituo vilivyoainishwa na Wizara ya Afya,Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kwa ajili ya kupata chanjo hiyo pamoja na
kubadilisha vyeti vipya.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage
wakati alipofika kupata huduma ya chanjo ya homa ya manjano ambayo inatolewa
bungeni hapa.
Waziri
Mwijage amesema duniani ugonjwa huu upo na zipo nchi nyingi ambazo zimepoteza
wananchi wake kwa kuugua ugonjwa huo“Suala hili ni muhimu sana kwa afya
zetu,pamoja na kwamba nchi yetu haina mgonjwa wa homa ya manjano.
Aidha
amesema maambukizi ya ugonjwa huu endapo mtu ataupata gharama za matibabu yake
ni ghali sana na inaweza kupelekea kupoteza maisha,hivyo ni vyema kujitokeza
kwa wingi kupata chanjo hiyo pamoja na kubadilisha kadi zao kwani usiweke
reheni maisha yako.
Hata
hivyo aliwatahadharisha wafanyabiashara,wanafunzi wale wanaosafiri au kusoma
nje ya nchi ni vyema wahakikishe wanapata chanjo hiyo kuliko kupewa kadi kwa
njia nyingine kwani kadi hizi zimeboreshwa na zina alama za siri ambazo nchi za
kimataifa zina uwezo wa kusoma alama zetu.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe.Mussa Zungu ameipongeza Wizara ya Afya,maendeleo
ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto kwa kubadilisha kadi hizi mpya kwa kuepukana na
vyeti vingi ambavyo vilikua vinanunuliwa mtaani bila kupata huduma za kupata chanjo,hivyo
ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha
wanapata chanjo hizo kwani ilikua ni hatari sana hususan nchi zile zenye
milipuko wa homa za manjano na hivyo kupata vyeti ambavyo ni halali.
Wizara
ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto limeongeza muda wa
kubadilisha vyeti vya zamani hadi mwisho wa mwezi huu na baada ya hapo vyeti
vya zamani havitatambulika tena.

Post a Comment