Mwenyekiti wa Kijiji cha IKUNGI avuliwa madaraka
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu
katikati akiwa na kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Haika Massawe na kaimu
mwenyekiti wa kijiji hicho Athuman Seleman wakiwa kwenye mkutano maalum wa
kijiji.
Mkaguzi wa ndani wa halmashauri ya
Ikungi Kitundu Mkumbo akisoma taarifa ya ukaguzi mbele ya mkutano maalum wa
kijiji cha Ikungi.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha
Ikungi waliohudhuria mkutano maalum wa kijijji hicho wakimsikiliza mkuu
wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu hayupo pichani.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha
Ikungi waliohudhuria mkutano maalum wa kijijji hicho wakimsikiliza mkuu
wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu hayupo pichani.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji
Mtaturu akizungumza na wananchi hawapo pichani kwenye mkutano maalum wa kijiji
cha ikungi,kulia kwake ni kaimu mwenyekiti wa kijiji hicho Athuman Seleman na
kushoto kwake ni kaimu mkurugenzi wa halmashauri Haika Massawe.
..........................................................................
MKUTANO maalum wa Kijiji cha Ikungi
wilayani Ikungi mkoani Singida umemuondoa Mwenyekiti wa kijiji hicho
Hussein Ikusi kutokana na matumizi mabaya ya madaraka kwa kufanya
ubadhirifu wa mali za kijiji zenye thamani ya shilingi milioni 9.
Ubadhirifu huo aliufanya toka
alipoingia madarakani mwaka 2014 akishirikiana na aliyekuwa mtendaji wa
kijiji hicho Hamis Isango aliyehamishiwa kijiji cha Irisya.
Hayo yalibainika baada ya
halmashauri ya kijiji kuitisha kikao maalum tarehe 24 aprili mwaka 2017
wakimtuhumu mwenyekiti kwa hoja zipatazo 5.
Hoja hizo ni kushindwa kusimamia mali
za kijiji,kushindwa kusimamia mipaka ya kijiji,kushindwa kuonyesha ushirikiano
na uongozi wa halmashauri ya wilaya,Ofisi ya mkuu wa wilaya na taasisi za
serikali zilizopo wilayani,kuwa chanzo cha migogoro badala ya kuwa mtatuzi na
kushindwa kusimamia usomaji wa mapato na matumizi ya kijiji kwa mujibu wa
sheria kwa kipindi cha miaka miwili na nusu.
Ubadhirifu huo umebainishwa na
mkaguzi wa mahesabu ya ndani Kitundu Mkumbo aliyeagizwa na mkuu wa wilaya hiyo
Miraji Mtaturu kufanya ukaguzi wa mapato na matumizi ya kijiji baada ya kupokea
tuhuma kuhusiana na mwenyekiti huyo.
Akizungumza katika kikao cha kutoa
taarifa kuhusiana na maamuzi yaliyoafikiwa na halmashauri ya kijiji Mtaturu
alimuagiza kaimu mkurugenzi wa halmashauri Haika Massawe kumsimamisha
kazi mtendaji wa kijiji cha Irisya Hamis Isango aliyehamishiwa kijiji
kingine ili arudi ikungi kujibu tuhuma za kuondoka na vitabu 12 vya kukusanyia
mapato alivyoshindwa kukabidhi wakati anahama ikiwemo na kutoa maelezo ya
fedha zilizoonekana kupotea mikononi mwake.
"Bwana Ikusi kabidhi
fedha na mali kama ushauri wa mkaguzi wa mahesabu alioutoa hapa mbele ya
wananchi"alisisitiza Mtaturu.
Aprili 24 mwaka huu halmashauri ya
kijiji iliazimia kwa kauli moja kumuondoa mwenyekiti huyo kutokana na
tuhuma hizo dhidi yake huku huku ikisisitiza kuwa Usimamizi wa Rasilimali
za Umma ni mabadiliko Chanya kwa maendeleo ya Ikungi.
Post a Comment