Shule za Binafsi Zimeongoza, Mitihani ya Utimilifu kwa Kidato Cha NNE
..........................................
Matokeo ya mtihani wa Utimilifu kwa wanafunzi wanaosoma kidato cha
nne katika shule za Sekondari za jiji la Dare es salaam yametolewa
leo jijini Dar es salaam yakiwa na alama za juu za ufaulu kwa wanafunzi
wanaosoma Katika shule zisizomilikiwa na Serikali.
Akitoa
matokeo hayo, Afisa Elimu wa Mkoa huo Bw.Raymond Mapunda amesema kuwa
ufaulu mzuri umeonekana zaidi katika shule Binafsi kuliko za serikali
kutokana na maandalizi mazuri yaliyofanywa na walimu wa shule hizo.
Amesema
kuwa licha ya mkoa wake kuwa na idadi ya walimu wa kutosha katika shule
zinazomilikiwa na Serikali bado wanafunzi wa kidato cha nne wa shule
hizo wamefanya vibaya ikilinganishwa na wale wanaosoma shule binafsi.
Amesema
mtihani huo ulifanyika Mei 25 hadi Juni 12,2015 mwaka huu na
ulihusisha shule 292 na kuongeza kuwa wanafunzi wapatao 40,356
walisajiliwa kufanya mtihani huo.
Bw.Mapunda
amesema kati ya hao 39,480 ambao ni sawa na asilimia 97.8 walifanya
mtihani huo huku 876 ambao ni sawa na asilimia 2.2 walishindwa kufanya
mtihani huo kutokana na sababu za ugonjwa na utoro.
Ameeleza
kuwa kutokana na idadi iliyosajiliwa, wanafunzi 37,560 wamefaulu
mtihani huo kulingana na madaraja mbalimbali yaliyoainishwa, huku idadi
kubwa ya wanafunzi wapatao 26,265 imeangukia katika daraja la mwisho la
ufaulu.
"Uchambuzi wa kina tulioufanya
umeonesha shule za Serikali zilizo nyingi zinazochukua wanafunzi 28,273
hazikufanya vizuri ikilinganishwa na shule Zisizo za Serikali zenye
idadi ya wanafunzi 11,207 hivyo Maafisa wa Elimu wa Manispaa waendelee
kufuatilia kwa karibu hali hii" Amesisitiza.
Aidha,
amezitaja shule kumi bora za Serikali zilizofanya vizuri kimkoa katika
mtihani huo kuwa ni pamoja na Jangwani,Pugu,Kisutu,Zanaki, Chang'ombe,Azania,Dar es salaam,KIbasila,Ilala na Benjamin Mkapa.
Kwa
upande wa Binafsi amesema ni pamoja Main Green Hill,Canossa ambayo
imeshika nafasi 5 mfululizo ikifuatiwa na Feza Boys nafasi 3 mfululizo
na shule ya Sekondari Alpha.
Ameongeza kuwa katika matokeo matokeo ya shule zote wasichana wameongoza kwa kuwa na ufaulu wa juu kuliko wavulana.
"Napenda
kuwafahamisha wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kuwa matokeo haya
yanaendelea kuchambuliwa kimasomo na kwa gredi na uchambuzi wote
utawekwa kwenye tovuti ya Mkoa wa Dar es salaam ya www.dsm.go.tz ili kilia mdau ,shule,mwalimu na mwanafunzi aweze kuyatumia.
Post a Comment