Profesa LIPUMBA na Hali ya Sintofahamu ndani ya Chama cha CUF
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wafuasi wa chama hicho waliojitokeza katika makao makuu yao yaliyopo Buguruni jijini Dar es salaam na kuwaambia CUF ni Taasisi hivyo wanachama wote wanatakiwa kukijenga chama hicho wawe na vyeo ama wasiwe na vyeo kazi kubwa ni kukijenga chama cha CUF amesema maneno hayo bila kufafanua.
Profesa Lipumba
alitakiwa kuzungumza na waandishi wa habari katika makao makuu hayo
lakini mpaka dakika za mwisho hakufanya mkutano huo badala yake alikuwa
na kikao na wazee wa chama hicho na baadhi ya viongozi wa dini na
wanachama na wakati akiondoka katika ofisi hizo ndipo akazungumza
maneno hayo hakuyafafanua zaidi.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim
Lipumba akisisitiza jambo wakati akizungumza na baadhi ya wanahabari
katika makao makuu ya CUF Buguruni jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wanachama wa chama cha
CUF wakiwa katika makao makuu ya chama hicho wakipiga kelele kuashiria
kumuunga mkono mwenyekiti wao Profesa Ibrahim Lipumba.
Wana CUF wakiwa wamejitokeza kwa
wingi katika makao makuu ya chama hicho Buguruni kumsikiliza Mwenyekiti
wao Profesa Ibrahim Lipumba.
Mpiga Picha wa Gazeti la
Uhuru Emmanuel Ndege akisaidiwa na waandishi wenzake mara baada ya
kujeruhiwa na feni wakati waandishi hao wakisubiri Mwenyekiti wa CUF
Profesa Ibrahim Lipumba kuzungumza nao katika makao makuu ya chama hicho
Buguruni.
Post a Comment