WILLIAM RUTTO – Hongera Rais KIKWETE kwa kukuza Tasnia ya Filamu Nchini Tanzania
Makamu
wa Rais Wa Kenya, Mh William Rutto akifungua maonyesho ya pili ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni Festival yajulikanayo kama
JAMAFEST kwa kuwakaribisha washiriki kutoka nchi zote za Afrika
Mashariki katika ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Kenyatta uliopo
jijini Nairobi, Nchini Kenya.
Makamu
wa Rais wa Kenya, Mh William Rutto akisaini kitabu cha wageni mara
baada ya kuwasili katika viwanja vya Ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Kenyatta kabla ya ufunguzi wa maonyesho ya JAMAFEST 2015.
Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Makamu
wa Rais wa Kenya, Mh William Rutto amempongeza rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mh Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuweza kukuza
tasnia ya filamu nchini Tanzania na kupelekea Wananchi wa Kenya na
Jumuiya ya Afrika Mashariki kupenda zaidi filamu za Kitanzania ambazo
zimekuwa na soko kubwa sana katika nchi za Jumuiya ya Mashariki.
Akizungumza
hayo wakati wa uzinduzi wa tamasha la Jumuiya ya Afrika Mashariki
Utamaduni lijulikanalo kama JAMAFEST 2015 linalofanyika katika viwanja
vya ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Kenyatta uliopo katika Jiji la
Nairobi Nchini Kenya, Makamu wa Rais wa Kenya, Mh Rutto pia aliwapongeza
marais wa nchi za Jumuiya Ya Afrika Mashariki kwa juhudi zao katika
Shughuli mbalimbali za kijamii, uchumi, utamadanu na Michezo.
Mh
Rutto alitoa pongezi kwa Rais Wa Rwanda, Mh Paul Kagame kwa kutoa
mchango mkubwa sana katika Michezo kwa kudhamini Michuano ya Kombe la
Kagame ambapo mwaka Huu Timu ya Azam FC kutoka Nchini Tanzania iliweza
kuibuka mshindi kwa kuifunga Timu yao ya Kenya Gor Mahia kwa mabao
Mawili kwa sifuri. Vilevile Mh Rutto aliipongeza timu ya Azam kwa kuweza
kuwa mabingwa wa Kombe la Kagame kwa kuweza kuifunga timu yao ya Kenya
ya Gor Mahia na kuweza kuibuka washindi wa Kombe la Kagame
linalodhaminiwa na rais wa Rwanda Nh Paul Kagame.
Mbali na Kumpongeza
rais wa Rwanda na Tanzania pia Makamu wa Rais wa Kenya, Mh William Rutto
aliwapongeza pia rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa kuwa mstari wa
mbele katika Kukuza utamaduni wa Nchi yake huku Rais wa Burundi
akipongezwa Kwa Kuweza kusakata kabumbu na kusema kuwa anatamani awe
rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA).
Maonyesho
ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni (JAMAFEST) yameshirikisha
nchini zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Kila Nchi mwanachama
wameweza kuonyesha Bidhaa zao pamoja na utamaduni wao. Maonyesho haya ya
JAMFEST hufanyika kila baada ya Miaka Miwili ambapo mwaka 2013
Maonyesho haya yalifanyika nchini Rwanda na mwaka huu yanaendelea
kufanyika Nchini Kenya huku mwaka 2017 maonyesho haya yanatarijiwa
Kufanyika Nchini Tanzania.
Post a Comment