Washiriki wa Mama SHUJAA WA CHAKULA Wamewasilisha Miradi ya Kilimo na Mazingira
Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 wakiwa katika Bwawa la Lamboni wakipata maelezo kutoka kwa wanakijiji hii ikiwa ni moja ya sehemu ya ziara yao jana.
Wenyeji pamoja na Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula wakielekea Mabondeni..Ilikuwa ni nafasi yao ya kufahamu maeneo mbalimbali Kijijini hapo.
Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa chakula wakioneshwa Madhari ya shule ya Msingi ya Kisanga na mmoja wa wanakijiji aliyesimama Mbele Kulia.
Hapa washiriki wa Shindano la Mama Shijaa wa chakula 2o15 linalo andaliwa na Oxfam kupitia kampeni yao ya Grow , kipindi kinachoruka kila siku ITV kuanzia Saa Kumi na mbili Jioni na Kurudiwa saa Tano na nusu asubuhi wakiwa katika ofisi ya Kusindika zao la Mihogo.
Hapa washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 msimu wa nne wakiwa katika moja ya kisima ambacho maji yake yananukia Mafuta, maji haya yanatumika zaidi katika shughuli za Kufulia Nguo.
Mwakilishi kutoka Oxfam Eluka Kibona aliyesimama (Kulia) akizungumza na Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Pamoja na wanakijiji katika Kijiji Cha Kisanga jana.
Kundi la kwanza la Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Mazingira..
Wanakijiji na Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasikiliza jinsi Miradi inavyo wasilishwa.
Kundi la pili la washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Kilimo Bora.
Kundi la Tatu la washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Kilimo Bora cha Mboga Mboga na Hihogo.
********
Ni siku nyingine tena katika kijiji cha Kisanga, jua la saa nne asubuhi ni kali huku mti huu mkubwa wa mkorosho uliopo eneo la makutano unatusitiri. Washiriki wa shindano la Mama shujaa wa Chakula Shindano lililiondaliwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow, walikuwa wamesimama vikundi vikundi, bila shaka walikuwa wanahadithiana chakula walichowapikia wenyeji wao jana.
Siku ya ilikuwa inaanza kwa waandaaji wa shindano kutengeneza makundi matatu ya kina Mama Shujaa wa Chakula watano watano.
Kwa muda watakaokaa hapa kijijini Kisanga, kila kundi
linatakiwa kutengeneza mradi wa maendeleo endelevu kwa manufaa ya kijiji
cha Kisanga. Ili kufahamu fursa na changamoto zilizopo, uongozi wa kijiji unawatembeza sehemu nne.
Upatikanaji wa maji ya uhakika kijijini hapa ni changamoto.
Kina Mama Shujaa wa Chakula wanaletwa sehemu hii yenye bwawa, wenyeji
wanaiita lamboni. Inasadikika kuwa zamani kulikuwa na kisima, ila kwa
sasa kimefunikwa na wingi wa maji. Pia kuna viumbe wakali kama vile
chatu.
Elimu ya msingi katika kijijini Napo inatolewa katika shule
ya msingi Kisanga. Wakina Mama Shujaa wa Chakula wanaoneshwa mandhari
ya shule na mwenyeji.
Wakazi wa kijiji cha Kisanga wanapata maji ya kunywa na
kupikia katika visima vilivyopo eneo hili linaloitwa Mfuru. Kufuatia
msimu wa mvua ulioisha, visima vyote vinne vina maji ya kutosha, japo
kisima kimoja maji yake hayatumiwi kwa kunywa kwani yana harufu
inayosadikika kuwa ni ya mafuta. Hata hivyo, wakati wa kiangazi kina
mama (wenyeji) wanalazimika kuamka saa tisa alfajiri kutokana na uhaba
wa maji, na kibaya zaidi usalama wao wakiwa njiani ni wa mashaka kwani
hawapewi msaada na waume zao (kwa walioolewa).
Ziara ya kutembelea kijiji inafika kwenye hospitali/kituo
cha afya cha Kisanga. Kina Mama shujaa wa chakula wanashangaa kuambiwa
bei kubwa ya matibabu katika kituo hicho, ambacho kwa siku ya leo
kimefungwa.
Zao kuu la Kisanga ni mihogo. Ziara ya kina Mama Shujaa wa
Chakula inaishia katika kituo cha kusindika mihogo. Hapa kunasagwa unga
wa mihogo, pia tambi na keki za unga wa mihogo zinatengenezwa hapa.
Naam, muda wa makundi kuwasilisha mapendekezo ya mradi wa
maendeleo endelevu waliopanga mbele ya wanakijiji wa Kisanga unawadia.
KUNDI LA KWANZA
Kutoa elimu juu ya mazingira, Kuchimba mashimo ya taka. Wafanyabiashara wanawake walio barabarani wafunike chakula
ili vumbi lisiingie.Wana Kisanga wote watahitajika kufanya usafi
jumamosi. Kuanzisha shamba darasa na kutoa elimu.
KUNDI LA PILI
Biashara cha mboga na matunda kwenye bonde (karibu na bwawa) kwa kutumia mbolea asili na maji yaliyopo. Kutoa elimu kwa kupitia shamba darasa jinsi ya kutumia rasilimali za kijiji kwa ajili ya maendeleo ya kijiji
KUNDI LA TATU
Mradi wa kilimo bora. Kilimo cha mbogamboga na kilimo cha mihogo na mahindi kwenye muinuko wa bonde. Wananchi kupewa elimu ya kilimo bora, kutumia wataalamu waliopo
Siku inaisha kwa waandaaji kupanga makundi matatu mapya ambayo watapewa kazi ambayo lazima iishe kesho hiyohiyo.
ILI KUMPIGIA KURA MSHIRIKI BOFYA HAPA>>>
ILI KUMPIGIA KURA MSHIRIKI BOFYA HAPA>>>
Post a Comment