Shirika la Nyumba NHC, limefanya Ukaguzi wa Miradi yake, MTWARA, RUVUMA , NJOMBE na MBEYA
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake akikagua mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na Shirika hilo eneo la Napupa Mjini Masasi.
Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Paul Mkami(kushoto) akimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake ramani ya eneo la ardhi lililopewa NHC kwa ajili ya kujenga nyumba za gharama nafuu Wilayani humo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakitembelea eneo la kujenga nyumba za gharama nafuu Wilayani Namtumbo alipofanya ziara yake katika Mkoa wa Ruvuma.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakikagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa Ofisi ya Shirika Mkoani Ruvuma ambapo ameagiza Ofisi hiyo iwe imekamilika ndani ya mwezi mmoja ili kuwapa fursa wateja na wananchi kupata huduma kwa urahisi. Kwa muda mrefu NHC haikuwa na Ofisi ya kudumu katika Mkoa wa Ruvuma kutokana na sguli za Mkoa huo kusimamiwa na Mkoa wa NHC wa Iringa.
Mradi wa nyumba za gharama nafuu unaojengwa na NHC Wilayani Makete nao ulipata fursa ya kutembelewa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake. Hapa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Mikoa Bw. Raymond Mndolwa anaonyesha eneo ambalo litajengwa Kituo cha biashara ili kuhudumia wakazi watakaoishi katika nyumba hizo za kisasa zinazouzwa kwa wananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC Bw. Haikamen Mlekio juu ya hatua za ukamilishaji wa mradi wa nyumba za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo alipotembelea mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwezi Septemba 2015.
Hali ya utekelezaji wa mradi wa nyumba za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo inavyoonekana hivi sasa.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakiukagua mradi wa nyumba za gharama nafuu unaotekelezwa na NHC Wilayani Mbarali.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakiwa na Viongozi wa TRA Mkoa wa Mbeya walipotembelea na kukagua maeneo yanayofaa kwa uwekezaji wa majengo ya biashara katika Mpaka wa Tanzania na Zambia –Tunduma. Taratibu zikikamilika NHC itajenga jingo la biashara katika mpaka huo maarufu na muhimu kiuchumi. Picha zote na Muungano Saguya.
Post a Comment