NAPE NNAUYE; " Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015 / 2020 Ipo Tayari "
Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi CCM akielekea kwenye ukumbi wa mkutano kwa ajili ya
kuzungumza na waandishi wa habari, huku akiwa ameshikilia kitabu cha
Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020 iliyopitishwa jana na Halmashauri Kuu
ya CCM mjini Dodoma.
........................................................................
Ilani hiyo inayotarajiwa
kuzinduliwa tarehe 25 Agosti ndiyo itakayotumika kwa kipindi cha miaka 5
ijayo iwapo Chama cha Mapinduzi CCM kitapewa ridhaa na wananchi
kuongoza nchi kupitia mgombea wake wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr. John Pombe Magufuli, katika uchaguzi mkuu ujao wa rais,
Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu kote
nchini Tanzania.
Katika Hatua Nyingine Nape amelaani na
kuzikanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya
magazeti kuandika kwamba Dr. John Pombe Magufuli alinukuliwa akisema
atagawa kwa kila mwalimu kompyuta moja na kila kijiji shilingi milioni
50 “Jambo hili ni uzushi mkubwa kwani Ilani ya Uchaguzi ilikuwa
haijakuwa tayari ndiyo imekamilika jana, Mambo hayo hakuna kwenye ilani
ya Uchaguzi ya CCM.“
Amefafanua na kuongeza kuwa
“Hizi ni njama za kufanya CCM ionekane imeanza kampeni mapema wakati
hatuwezi kufanya hivyo na tunajua sheria na taratibu za uchaguzi”.
Mkutano huo umefanyika katika Makao makuu ya CCM Ofisi ndogo Lumumba
leo.
Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi CCM akitolea ufafanuzi mambo mbalimbali kwa waandishi
wa habari wakati akizungumza nao kwenye mkutano uliofanyika CCM Lumumba
jijini Dar es salaam.
Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi CCM akiionyesha ilani ya uchaguzi iliyopitishwa jana
na Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.
Hii ndiyo Ilani yenyewe...
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wapiga picha vyombo mbalimbali vya habari wakichukua matukio katika mkutano huo.
Post a Comment