|
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward
Lowassa na Mkewe, Mama Regina Lowassa wakifanyia Ibada ya kimila na
Wazee (Malaigwanani) ya Kimasai, wakati wa Mkutano wa kutafuta wadhamini
wa Tume ya Uchaguzi pamoja na kutambulishwa kwa wananchi, uliofanyika
Agosti 15, 2015, kwenye Uwanja wa Kimandolu, Jijini Arusha. | |
|
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward
Lowassa akipokea rungu maalum ikiwa ni ishara ya Uongozi, kutoka kwa
Mzee Nyinyajwangwa Laiza, mara baada ya Ibada
ya kimila na Wazee (Malaigwanani) ya Kimasai, wakati wa Mkutano wa
kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi pamoja na kutambulishwa kwa
wananchi, uliofanyika Agosti 15, 2015, kwenye Uwanja wa Kimandolu,
Jijini Arusha. |
|
Mzee wa Kimasai (Laigwanani), Mzee Naftar Samson Mollel akiongoza
ibada ya kimila na kumtambulisha rasmi kwenye ukoo, Mgombea Mwenza wa
Urais wa UKAWA kupitia CHADEMA, Dkt. Juma Haji Duni ambaye sasa anaitwa
Juma Duni Ole Laiza. |
|
Muasisi Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee Edwin
Mtei akizungumza na maelfu ya wananchi wa Jiji la Arusha, wakati
akimtambulisha Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa,
wakati wa Mkutano wa kutafuta udhamini wa Tume ya Uchaguzi na
kutambulishwa kwa Mgombea huyo na Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni,
uliofanyika kwenye Uwanja wa Kimandolu, leo Agosti 15, 2015. |
|
Muasisi Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee
Edwin Mtei akipena mkono na Mgombea Mwenza wa Urais wa UKAWA kupitia
CHADEMA, Dkt. Juma Haji Duni.
|
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mh. Godbless Lema akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa hadhara wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi wa Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,pamoja na kutambulishwa kwa wananchi, uliofanyika Agosti 15, 2015, kwenye Uwanja wa Kimandolu, Jijini Arusha.
|
Mgombea wa Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, akihutubia wananchi. |
Post a Comment