EDWARD LOWASSA AREJESHA FOMU YA URAIS MAKAO MAKUU YA CHADEMA
WAZIRI Mkuu wa zamani Mh. Edward
Lowassa, akipungia wafuasi wa CHADEMA na wananchi wengine waliofurika
makao makuu ya chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi
Agosti 1, 2015, baada ya kurejesha fomu za kukiomba chama chake kumteua
kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi
mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa ndiye
atakayesimama kwa niaba ya vugucugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi
UKAWA.
Na Mwandishi wetu
WAZIRI
Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa, ambaye leo Jumamosi Agosti 1, 2015
amerejesha fomu za kuomba chama chake kipya cha CHADEMA, kimteue kuwania kiti
cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya vyama vinavyounda
vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi maarufu kama UKAWA, ameanza na mtaji wa
“kura” zaidi ya Milioni 1.6, Mkurugenzi wa Oganaizesheni, mafunzo na
msimamizi wa Kanda 10 za chama hicho, Benson Kigaila ametangaza.
Kigaila
amesema, idadi hiyo ni ya wanachama wa CHADEMA na wananchi wengine ambao
wamemdhamini katika fomu zake za kuomba kuteuliwa na chama hicho.
“Wote
waliomdhamini, kwakuwa walikuwa wengi nchi nzima, tulitoa masharti kuwa kila
anayetaka kufanya hivyo awe na kadi ya kupigia kura na aweke namba yake ya simu
ya mkononi na wote wamefanya hivyo na hii ina maana kuwa CHADEMA, chini ya
UKAWA, tuna kura za Rais milioni 1,662, 397.” Alifafanua Kigaila, wakati
akielezea utaratibu uliotumika wa wana CHADEMA kumdhamini Mh. Lowassa.
Hatua
hiyo ya Mh. Lowassa, ya kurejesha fomu zilizopokelewa na Makamu Mwenyekiti wa
chama hicho Tanzania Bara, Profesa Abdallah Safari, inasubiri hatua nyingine ya Kamati
Kuu ya chama hicho ambayo inakutana Agosti 2, 2015 ili kuzipitia fomu hizo
kuona kama zinakidhi matwaka ya kikatiba na kanuni za chama hicho kabla ya
kupelekwa kwenye vikao vingine vya juu na hatimaye kwenye mkutano mkuu
unaotarajiwa kufanyika Agosti 4, 2015 hapa jijini Dar es Salaam.
Wafuasi wa CHADEMA, wakimshangilia Mh. Lowassa, alipokuwa kitoka kwenye makao makuu ya chama hicho baada ya kurejesha fomu.
Mh. Lowassa, akikabidhi fomu hizo, kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Tanzania Bara), Profesa Abdallah Safari.
Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Kanda 10 za CHADEMA, Benson Kigaila, akionyesha lundo la fomu zilizomdhamini Mh. Lowassa.
Mh. Lowassa, akipongezwa na Mjumbe wa
Kamati Kuu ya CHADEMA, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani ya
chama hicho, Mabere Nyaucho Marando.
Wabunge wa CHADEMA na majimbo yao
kwenye mabano kutoka kushoto, Godbless Lema (Arusha Mjini), Wenje
(Nyamagana), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Mchungaji Peter Msigwa
(Iringa Mjini).
Mh. Lowassa, akiwasili makao makuu ya CHADEMA.
Mh. Lowassa, akiwa na Esther Bulaya.
Profesa Safari.
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, (Zanzibar), Salum Mwalimu.
Mtoto wa mwisho wa Mh. Lowassa,
(katikati), akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na
viongozi wa CHADEMA, wakati baba yake Mh. Lowassa aliporejesha fomu.
Wabunge na viongozi wa CHADEMA.
Vijana wa 4U ambao walimuunga mkono Mh. Lowassa wakati akiwa CCM, na sasa wanaendelea kumuunga mkono akiwa CHADEMA.
Wananchi waliofurika makao makuu ya CHADEMA wakati Mh. Lowassa akirejhesha fomu.
Mh. Lowassa, akiteta jambo na Afisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene.
Post a Comment