Header Ads

Kikao cha Halmashauri kuu ya CCM - Dodoma

 
Mwenyekiti wa CCM, Rais JAKAYA KIKWETE

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Rais Jakaya Kikwete amesema uchaguzi mkuu mwaka huu, lazima chama hicho kihakikishe kinateua wagombea wanaouzika na kukubalika kwa wananchi kwa ngazi zote kuanzia udiwani, ubunge na urais huku akitaka chama hicho kusoma alama za nyakati.

Rais Kikwete amesema hayo leo mjini wakati anafungua kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho kiliachoanza kikao chake cha siku mbili leo jioni ambapo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia mchakato wa uchaguzi mkuu. 

Amesema kuwa wajumbe wa halmashauri kuu wahakikishe wanachagua mgombea anayekubalika kwa wananchi huku akiendelea kufafanua kuwa wana CCM wapo milioni sita lakini watanzania wanaopiga kura ni milioni 23.

 “Msipochagua watu wanaokubalika na kuuza kwenye uchaguzi mkuu mtajikuta mnashindwa hata kuwa chama cha kwanza cha upinzani kutokana na matokeo mabaya mtakayoyapata,”alisema Rais Kikwete. 

Amesema CCM itambue kuwa kama wao watapitisha jina la mgombea kwasababu ya kuogopana , basi wananchi hawatawaogopa na watachagua mtu kulingana na mahitaji yao. 

 Amewakumbusha wana CCM usemi wa Mwalimu Julius Nyerere kwamba Rais anaweza kutoka chama chochote lakini Rais bora atatoka CCM.

No comments

Powered by Blogger.