Ripoti za Ki-michezo kutoka TFF
Akiongea wakati wa kusaini mktaba
huo mpya, Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya simu ya Vodacom Kelvin
Twissa, amesema kampuni yao inafurahia kuendelea kuwa sehemu ya udhamini
ya ligi kuu nchini, mafanikio ya timu bora na kufanya vizuri katika
michuano ya kimataifa inatokana na kuwa na ligi bora ambayo inadhaminiwa
na Vodacom.
Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi
amewashukuru kampuni ya Vodacom kwa kukubali kuendelea kuidhamini ligi
kuu kwa kipindi kingine cha miaka mitatu (3) na kuongeza sehemuya
udhamini wao kwa asilimia 40%.
Tunaishukuru kampuni ya Vodacom
kwa kuendelea kuwa sehemu ya mafanikio ya mpira wa miguu nchini,
udhamini wanaotupatia unavisaidia vilabu kujiandaa na kujiendesha na
mikikimikiki ya ligi na kuifanya ligi kuwa na ushindani wa hali ya juu,
msimu huu ligi itakua na timu 16 tunatarajia kuendelea kushuhudia uhondo
huo chini ya udhamini wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
Mkataba huo mpya wa udhamini kwa
kipindi cha miaka mitatu, umeboreshwa na kuwa na ongezeko la asilimia
40% kutoka katika mkataba wa awali uliomalizika.
Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 12, 2015.
TFF YAMPONGEZA JAJI MAMBI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Makamu Mwenyekiti wa
Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Adam Mambi kwa kuteuliwa kuwa Jaji wa
Mahakama Kuu nchini.
Katika Salam zake kwa Jaji Mambi,
Malinzi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta
Jakaya Kikwete kwa kumteua mwanafamilia huyo wa mpira wa miguu nchini
kushika wadhifa huo.
TFF kwa niaba ya familia ya mpira
wa miguu na watanzania wote inamtakia kila la kheri Jaji Adam Mambi
katika majukumu yake mapya ya Ujaji katika Mahakama Kuu nchini Tanzania.
TRA KUENDESHA SEMINA YA KODI
Mamlaka ya Kodi na Mapato nchini
(TRA) inatarajiwa kuendesha semina ya kodi kwa viongozi wa vilabu
viliyopo jijini Dar es salaam, siku ya ijumaa tarehe 14 Agosti katika
hoteli ya Tiffany iliyopo eneo la Kisutu.
TRA itaendesha semina hiyo kwa
vilabu vilivyopo ligi kuu, ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili
ambapo viongozi wakuu wa vilabu hivyo, Katibu Mkuu, Mwenyekiti, na
Mhasibu wanapaswa kuhudhuria semina hiyo.
Kwa kuanzia TRA itaendesha semina
hiyo jijini Dar es salaa, na baadae kuendelea na semina hizo kwa vilabu
vilivyopo mikoani kwa lengo la viongozi wa vilabu kutambua umuhimu wa
ulipaji kodi kwa wachezaji, makocha wanaowaajiri katika vilabu vyao.
Semina hiyo itaanza saa 3 asubuhi
mpaka saa 5 kamili asubuhi katika hoteli ya Tiffany iliyopo eneo la
Kisutu jijini Dar es salaam, vionggozi wa vilabu vya ligi kuu, ligi
daraja la kwanza, ligi daraja la pili waliopo jijini Dar es salaam
mnaombwa kuhudhuria semina hiyo.
Post a Comment