Mzozo wa Mgodi wa Marikana, Familia Kuishitaki Serikali ya Afrika Kusini
Familia za wachimbaji mgodi 37
waliouawa na polisi nchini Afrika Kusini wakati wa mgomo mnamo 2012
wamewasilisha kesi dhidi ya serikali.
Jamaa hao wanadai malipo kwa kupoteza kipato, na gharama za hospitali kutokana na mshtuko wa kiakili na kihisia.
Wanataka
pia waziri wa idara ya polisi aombe msamaha rasmi kwa kuwapoteza jamaa
zao waliokuwa wakifanya kazi katika mgodi wa madini ya Platinum wa
Marikana katika jimbo lililopo kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Ripoti iliyosubiriwa kwa muda mrefu kuhusu mauji hayo iliyotolewa Juni
iliwalaumu kwa pamoja wamiliki mgodi huo Lonmin maafisa wa polisi pamoja
na vyama vya wafanyakazi kwa mauaji hayo.
Post a Comment