Serikali Kuwalipa Fidia Walioathirika na Wanyapori
Naibu Waziri wa
Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akikagua moja ya shamba la mahindi
lililoharibiwa na tembo katika kijiji cha Kunzugu, wilaya ya Bunda Mkoani Mara jana
wakati wa ziara yake ya kuangalia changamoto za uhifadhi mkoani humo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda,
Lydia Bupilipili.
Naibu Waziri wa
Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Kunzugu, wilaya ya Bunda, mkoani Mara jana alipotembelea moja ya shamba la
mahindi lilioharibiwa na tembo wakati wa ziara yake ya kuangalia changamoto za
uhifadhi mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia
Bupilipili.
..............................................
..............................................
NA HAMZA TEMBA - WMU
Serikali
kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema italipa madeni yote ya miaka ya
nyuma ya vifuta jasho na vifuta machozi ambayo inadaiwa na wananchi waliokubwa
na vitendo vya uharibifu wa wanyamapori nchini kabla ya bunge lijalo la
bajeti, madeni hayo ni yale ambayo yameshaifikia wizara hiyo na
kuhakikiwa.
Akizungumza
jana na uongozi wa wilaya ya Bunda wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku
moja ya kufuatilia changamoto za uhifadhi wilayani humo, Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani amesema uamuzi huo wa Serikali
utaondoa kilio cha muda mrefu cha wananchi ambao wamepata madhara mbalimbali ya
wanyamapori ikiwemo vifo, majeruhi, kuliwa mazao na kuharibiwa mashamba
yao.
"Serikali
ya awamu ya tano imeshakamilisha takwimu za madai, yale yote tunayodaiwa huko
nyuma, yaliyoifikia Wizara yakafanyiwa uhakiki na nimesema kwenye uhakiki huo
ndani ya kipindi cha miaka kumi, kwa wilaya zaidi kidogo ya 80 ambazo ndizo
zina changamoto hizi kwa kiwango kikuu, deni jumla ni shilingi 2,081,532,700
(bil. 2.9)", amesema.
Amesema
wilaya ambazo zimeathirika zaidi na vitendo hivyo na ambazo madai yao ni
makubwa zaidi ya Wilaya zingine ni Serengeti na Bunda ambazo ziko mkoani Mara
na zinapakana na Hifadhi ya taifa ya Serengeti, Ziwa Victoria, Pori la Akiba
Grumeti na Ikorongo. "Serengeti ndiyo inayoongooza kwa madai hayo,
shilingi milioni 408,547,600 alafu Bunda shilingi milioni
265,969,750",.
Pamoja
na Serikali kujiwekea utaratibu huo na wananchi wa kulipa vifuta jasho na
vifuta machozi kwa waathirika, amesema ipo haja ya kutafuta njia endelevu ya
kukabiliana na changamoto hizo na fedha ambayo ingetumika kulipia fidia hizo
ikatumika kuwezesha mpango huo endelevu. Amesema mpango huo utawezekana kwa
kuwashirikisha wananchi.
Ili
kufanikisha mpango huo ameuagiza uongozi wa wilaya ya Bunda na Serengeti
kuratibu ushiriki wa wananchi wao katika zoezi hilo kwa kuunda vikundi
shirikishi katika kila kijiji, kubaini mahitaji yake ikiwemo vifaa na
kuwasilisha taarifa hiyo wizarani kabla ya tarehe 15 januari mwaka huu, kwa
ajili ya hatua zaidi za kufanikisha mpango huo.
Amesema
ushirikiano huo pekee hautoshi kukabiliana na changamoto hizo kama wananchi nao
hawataipunguzia mzigo serikali wa kupambana na vitendo vyao viovu dhidi ya
uhifadhi, ili nguvu hiyo itumike katika kushirikiana nao kwenye ulinzi dhidi ya
wanyama waharibifu. "Wananchi waache vitendo viovu dhidi ya uhifadhi,
ujangili, kuua wanyamapori",.
Ameeleza
kuwa miongoni mwa sababu za kuongezeka kwa changamoto hizo ni matokeo ya tabia
za wananchi kusogelea maeneo ya hifadhi kwa ajili ya shughuli za kibinadamu,
jambo ambalo lina athari kubwa katika uhifadhi na usalama wa wananchi wenyewe,
hivyo ni lazima liepukwe.
"Njia
ambayo tembo alikua akipita miaka 20, 30, 40 ndo anapita kila siku, sisi
tumeenda kujenga, tumeenda kulima mashamba, sasa tembo wao na wenyewe wana
ownership (umiliki), ile njia wao wanaona ni ya kwao tu, kwahiyo akikutana na
wewe anafanya hayo anayoyafanya, hata kwenda kukaa kufanya shughuli za
kibinaadamu ikiwemo kujenga na kulima jirani kabisa na kwenye mpaka ya hifadhi
na yenyewe ni tatizo".
Naibu
Waziri Makani amehitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Mara jana ambapo
alitembelea vijiji kadhaa wilayani Bunda na Serengeti na kushudia athari
mbalimbali za uharibifu wa wanyamapori pamoja na kupokea malalamiko mbalimbali
ya uharibifu huo kutoka kwa wananchi. Alishuhudia mashamba kadhaa ya mahindi
yaliyokuwa karibu na maeneo ya hifadhi yakiwa yameharibiwa na tembo.
Post a Comment