Bodi ya Filamu yatoa Mafunzo Kwa Zaidi ya Wasanii 300 Jijini Mwanza
Katibu Tawala Msaidizi, kitengo cha elimu mkoani Mwanza, Khamis Maulid, akifungua warsha ya mafunzo ya filamu ya siku tatu mkoani Mwanza iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini kwa ajili ya Wasanii wa Filamu mkoani Mwanza.
..........................
Maulid amesisitiza wasanii hao kuhakikisha wanatengeneza filamu zenye ubora na zinazozingatia maadili ya mtanzania na kukaguliwa kabla ya kuingia sokoni hatua ambayo itasaidia kukuza soko la filamu mkoani Mwanza.
Pamoja na mambo mengine, warsha hiyo imelenga kuwawawezesha kielimu wasanii wa filamu mkoani Mwanza kutengeneza filamu zenye ubora, namna ya uanzishwa wa vikundi na kampuni za filamu, uandishi wa miswada ya filamu,uongozi wa filamu pamoja na taaluma ya upigaji picha.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo, akielezea majukumu ya bodi hiyo ambayo ni pamoja na kuhakikisha ubora wa filamu pamoja na hakimili za wasanii wa filamu nchini.
Wasanii wa filamu mkoani Mwanza wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo, wakati wa warsha kwa wasanii hao hii leo.
Afisa Uendeshaji na Maso kokutoka Mfuko wa Pensheni PPF akielezea umuhimu wa wasanii wa filamu mkoani Mwanza kujiunga na mfuko huo ili kunufaika na mafao kutokana na kazi zao za sanaa.
PPF ni miongoni mwa wadau waliosaidia kufanikisha warsha ya mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini.
Post a Comment