Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Meneja wa Wakala
wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Kagera Eng. Andrea Kasamwa wakati
alipokagua athari za tetemeko la ardhi lililoikumba miundombinu ya barabara
mkoani humo.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amekagua athari za tetemeko la
ardhi lililoikumba miundombinu ya barabara katika mkoa wa Kagera na kujionea
athari zilizojitokeza katika mkoa huo.
Prof. Mbarawa
amejionea athari za tetemeko la ardhi katika barabara ya Rwamishenye hadi
Bandari ya Bukoba yenye urefu wa KM 4.6 ambayo imeathirika mita 60 na barabara
ya Bukoba-Mtukula yenye urefu wa KM 80 ambayo imeathirika kwa mita 200 na kusisitiza
kwamba Wizara yake itatekeleza maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu Mhe.
Kassim Majaliwa ili kukabiliana na changamoto zilizojitokeza.
“Tunatoa pole kwa
wananchi wa mkoa wa Kagera kutokana na maafa yaliyojitokeza hivyo tutafanyia
kazi maelekezo ya ukarabarati wa miundombinu iliyoathiriwa na tetemeko kadiri
tulivyoelekezwa na Waziri Mkuu”, amesema Prof. Mbarawa.
|
Post a Comment