DAVID KAFULILA aongoza Mahafali ya Darasa la Saba Shule ya Msingi GOSHEN
Mwanafunzi Eugene Kephasi, akimvika skafu, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maafali ya saba ya darasa la saba katika Shule ya Goshen Nursery and Primary School Bunju jijini Dar es Salaam leo mchana.
David Kafulila akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Shule hiyo, Nipael Mrutu wakati akipewa historia fupi ya shule hiyo kutoka kwa Mkuu wa Shule hiyo, Felister Mrutu (hayupo pichani).
Kafulila (katikati) na viongozi wa shule hiyo wakielekea meza kuu tayari kwa maafali hayo, Kutoka kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Felister Mrutu, Mkurugenzi wa Shule, Nipael Mrutu, Lupi Kiyabo na Mchungaji Elisifa Kephasi.
Na Dotto Mwaibale
MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila amesema urithi pekee wa watoto ni elimu na sio mali kama ilivyozoeleka.
Kafuli ametoa kauli hiyo katika maafali ya saba ya darasa la saba katika Shule ya Goshen Nursery and Primary School Dar es Salaam leo mchana.
"Napenda kuwaomba wazazi na walezi kuendelea kuwapa elimu watoto wenu kwani ndio msingi wa maisha yao badala ya kuwarithisha magari, nyumba na vitu vingine vya thamani" alisema Kafulila,
Kafulila ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maafali hayo alitoa shukurani zake kwa uongozi mzima wa shule hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwaandaa wanafunzi hao ambao watakuja kuwa wataalamu na viongozi wa baadae.
Mkuu wa Shule hiyo, Felister Mrutu alisema shule yao imekuwa ikipokea wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali bila ya kujali dini wala uraia na inazingatia maadili jambo linalowavutia watu wengi kuwapeleka watoto wao wakiwemo wa kutoka nje ya nchi.
Katika maafali hayo wanafunzi wa shule hiyo walionesha burudani mbalimbali kama kuimba, gwaride, sarakasi, karate na michezo mingine ya ukakamavu waliyofundishwa na vijana kutoka chama cha Skauti Tanzania.
Post a Comment