Kiwanda cha kutengeneza nguo cha Nida Textile Industries kilichopo Tabata Jijini Dar es Salaam kimetozwa
faini ya shilingi milioni Thelathini kwa kosa la uchafuzi w a mazingira kwa
kutiririsha maji taka na yenye sumu katika mto kibangu kuhatarisha maisha ya
mazingira na viumbe hai pamoja na kiwanda
hicho kuwa na mazingira machafu na hivyo kuatarisha maisha ya wafanyakazi
kiwandani hapo.
Faini hiyo inayotakiwa kulipwa ndani ya siku saba kwa Baraza
la Taifa na Hifadhi na Usimamizi waMazingira NEMC imetokana na ziara ya Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ya
kukagua viwanda na mazingira nchini ambapo sambamba na adhabu hiyo kiwanda
hicho kimetakiwa kufanya usafi mara moja katika mazingira kiwandani hapo,
pamoja kupeleka repoti ya upimaji wa moshi, vumbi litokanalo na makaa ya mawe
na maji yanayotoka kiwandani hapo ili serikali kujiridhisha kama si hatarishi
kwa mazingira.
‘’Ili kujiridhisha NEMC waje nao wachukue vipimo vya maji
haya yanayotiririka ili tuone kama ni salama kwa mazingira na viumbe hai, na
kiwanda kiwasilishe cheti cha utirishaji maji kwa Baraza.” Alisisitiza Naibu
Waziri Mpina.
|
Post a Comment