Wadhamini waogopa kufadhili Soka la Wanawake Nigeria
Wadhamini nchini Nigeria wanaogopa kuzifadhili timu za soka za wanawake kutokana na dhana potovu kwamba timu hizo hufananishwa na 'wapenzi wa jinsia moja' kiongozi mkuu wa shirikisho la soka nchini Nigeria amesema.
Naibu wa rais wa shirikisho la soka la Nigeria ,Seyi Akinwunmi, alikuwa anafafanua maoni yake baada ya kunukuliwa akiwalaumu wapenzi wa kike wa jinsia moja kwa upungufu wa makali kwa timu hiyo ya kitaifa.
Timu hiyo kwa jina The Super Falcons ni timu kutoka Afrika yenye mafanikio ya kitaifa. Uhusiano wa wapenzi wa jinsia moja ulipigwa marufuku nchini Nigeria.
Nigeria ni nchi ambayo isiyopenda mabadiliko ,wapenzi wa jinsia moja hulalamikia kubaguliwa.
Naibu wa rais wa shirikisho la soka la Nigeria (NFF) Bwana Akinwunmi, amenukuliwa akisema 'wapenzi wa jinsia moja huuwa timu.
Post a Comment