Header Ads

Taswira ya Leo Kutoka Ndani Bunge Mjini DODOMA

 Mbunge wa Viti Maalumu, Bupe Mwakang'ata (CCM), Mkoa wa Rukwa, akiuliza swali kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) bungeni Dodoma LEO, kwamba serikali ina mkakati gani wa kusimamia fedha asilimia 10 zinazotolewa na Halmashauri kwa ajili ya maendeleo  vijana na wanawake.

 Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson akiongoza kikao cha Bunge cha majadiliano ya Bajeti ya Serikali bungeni Dodoma.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiswali la ni lini ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Nyamagana Mwanza utamalizika. Swali hilo lililulizwa na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula.

 Mbunge wa Kalenga, Godfrey Mgimwa akiuliza swali bungeni.

 Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Makame Mabrawa akijibu maswali ya wabunge.

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Edwin Ngonyani akijibu maswali ya wabunge.


 Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu akiuliza swali bungeni.

 Wageni waalikwa wakiwa bungeni dodoma.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge Bwanausi wa Lulindi.

 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Yusufu Hamad Masauni bungeni.

 Familia ya Mbunge wa Mafinga Cosato Chumi ikiwa bungeni Dodoma huku ikifuatilia mwenendo wa Bunge.

 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St Marys Duluti ya Arusha wakiwa bungeni kufuatilia menendo wa Bunge hilo.

 Mbunge wa Viti Maalum, Jasmine Tisekwa akichangia mjadala wa serikali.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Mary's Duluti ya Arusha waliotembelea Bunge, Dodoma.

 Wabunge wa upinzani wakitoka bungeni kikao cha jioni kwa kutokuwa na imani na Naibu Spika.

No comments

Powered by Blogger.