Wadau wa Ufugaji, Kilimo na Uvuvi watoa Maoni Kuhusu Mpango wa Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2016 / 2017
Na Mwandishi wetu
Wakulima wadogo wadogo zaidi ya 45 katika harakati za maendeleo
nchini na sekta za uvuvi, na ufugaji kutoka mikoa mbalimbali nchini
wamekutana jijini Dar es salaam katika kujadili mwongozo wa kuandaa mpango na
bajeti ya serikali 2016/2017.
Warsha hiyo ambayo imeandaliwa na ushirikino wa mashirika matano ambayo ni Oxfam, Policy Forum, ANASAF,
Action Aid na TGNP zaidi ikiwa ni kuwaleta pamoja wakulima hao wadogowadogo katika
kupitia mwongozo na kuujadili kwa ukaribu pamoja na kuuchambua kwa kina zaidi.
Wakati akitoa majumuisho kutoka
ukurasa wa 14-20 Bi Flora Mathias Kutoka Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkulima
mdogo ameomba Mkulima ameiunga mkono hoja ya mwanamke kuthaminiwa na kupata
nafasi ya kuuza Bidhaa zake, kupewa nafasi ya kujitambua na kumiliki Ardhi,
huku akiulalamikia mwongozo huo wa bajeti elekezi kutoweka wazi kuhusu mfuko wa
wanawake katika kusaidia uzalishaji na kuomba bajeti inayokuja izingatie hilo.
Mzee Namagono Hassan kutoka kundi
la wakulima ametoa maelezo kutoka
ukurasa wa 6-9 kuhusu mambo muhimu katika mwongozo wa Bajeti 2016/17,
kuwa pamoja na kuanzishwa kwa Benki ya wanawake, isitazame tuu wanawake wa
mjini bali na vijijini kwani wao ndio
wazalishaji zaidi wa Chakula kuliko waishio mijini.
Kwa upande wake Datius Pastory
Inshansha Mwanaharakati na Mkulima mdogo ukurasa wa 20-23 amepitia ukurasa 23-24 unaotoa
maelekezo mahsusi kwa sekretarieti za mikoa na mamlaka ya serikali za mitaa na
kushauri kuwepo uwazi wa mapato na matumizi ya Serikali za Mitaa, pia Bajeti
ielekezwe zaidi vijijini kulipo mjini na kudhibiti fedha za uvuvi,kilimo na
ufugaji zisiishie kwa watu wachache bali wahusika kwa ujumla.
Maelezo mengine yametolewa na Bwana
Adam Simwinga kuhusu ukurasa wa 9-15 kipengele cha Maelekezo ya Maandalizi ya
bajeti kwamba amegundua hakuna mkakati wa kuongeza mapato kupitia simu, mkakati
wa msamaha wa kodi, hivyo wameshauri kilimo kiwe ni sehemu ya eneo wezeshi na
malighali katika viwanda nchini Tanzania na katika mpango wa maendeleo na
kuongeza kuwa asilimia 30% hazijitoshelezi kukuza sekta ya kilimo nchini.
Wanaharakati hao wameishauri
serikali kutowasahau katika kuwawezesha mikopo ili kukuza sekta zao kimaendeleo
huku wakilalamika wakulima
kutoshirikishwa kikamilifu.
“Tunaomba mkopo wa Magari ya
wabunge upungue kutoka Mil 90 hadi Mil 20 ili zile mil 70 zitumike katika
shughuli zingine za maendeleo ikiwemo na kilimo na pia kuwe na viwanda vidogo
vidogo katika mikoa mbalimbali mfano kiwanda cha Machungwa” aliongeza Bi.
Kidani Mhenga wanajadili ukurasa wa 3-5 mapitio ya uchumi na utekelezaji wa
Bajeti.
Bi.
Kidani Mhenga kutoka kikundi namba tatu ambao walikuwa wanajadili
ukurasa wa 3-5 mapitio ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti za Serikali
kuoka katika mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017.
Mzee
Namagono Hassan Kutoka kikundi namba moja akitoa maelezo kutoka katika
mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017
kutoka ukurasa wa 6-9 unaoelezea mambo muhimu katika mwongozo wa Bajeti
2016/17.
Bi
Flora Mathias Kutoka Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkulima mdogo akitoa
majumuisho kutoka kipengele cha namna ya kudhibiti Bajeti za Serikali
kutoka katika mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka
2016/2017 ukurasa wa 14-20, picha ya juu ni wanakundi wakiwa wanajadili
swala hilo. Picha ya juu ni baadhi ya mama Shujaa wa chakula ambao
wanatoka katika Kampeni ya Grow inayoendeshwa na Oxfam Tanzania pamoja
na wadai wengine wa kilimo.
Bwana
Adam Simwinga akitoa maelezo kutoka kundi namba mbili ambao walikuwa
wachambua mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017 ukurasa wa
9-15 kipengele cha Maelekezo ya Maandalizi ya bajeti.
Datius
Pastory Inshansha ambaye ni Mwanaharakati na Mkulima mdogo mdogo
akiwasilisha kundi lake la Tano ambao walikuwa wanajadili ukurasa wa
20-23 kutoka katika mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya Serikali kwa
Mwaka 2016/2017 inayozungumzia maelekezo mahsusi kwa sekretarieti za
mikoa na mamlaka ya serikali za mitaa.
Baadhi ya wakulima, wafugaji na wavuvi wakiendelea na mjadala.
Picha na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa
Post a Comment