KITUO CHA UTAFITI CHA RCRSDS KUZINDUA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA KUKUSANYA, KUHIFADHI NA KUWEKA ANGANI TAARIFA ZA KITAFITI ZA UWAJIBIKAJI WA TAASISI ZA BINAFSI NA UMMA
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Utafiti wa Shughuli za Maendeleo ya Jamii
Tanzania (RCSDS),Abraham Shempemba (kulia) akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari, Dar es Salaam leo , kuhusu mafanikio ya tafiti zao
walizozifanya zinazoonesha takwimu za misaada iliyotolewa kisekta,
gharama zilizotumika, uwajibikaji wa jamii na jinsi ilivyonufaika.
Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kituo hicho, Chrizostom Thadeo.
…………………………………………………………………………………..
Celina Mathew
KITUO cha Utafiti wa shughuli za
maendeleo ya jamii Tanzania(RCSDS), kinatarajia kuzindua mfumo wa
kielektroniki wa kukusanya, kuhifadhi na kuweka angani taarifa za
kitafiti za uwajibikaji wa taasisi za binafsi, za umma na watu binafsi
serikali kuu na za mitaa na hata mtu mmoja mmoja.
Mfumo huo unatarajiwa kuzinduliwa
mwishoni mwa mwezi huu ambapo utapelekwa katika mikoa 30 Tanzania Bara
pamoja na maeneo 100 yenye wananchi wenye uhitaji mkubwa.
Akizungunza Dar es Salaam jana,
Mkurugenzi wa kituo hicho, Abraham Shempemba alisema lengo la mwendelezo
huo ni kutoa nafasi kwa walengwa kutambua mchango unaotolewa kwao na
wadau mbalimbali pamoja na misaada kwa jamii zenye uhitaji mkubwa.
“Sisi kama RCSDS tunatambua uwepo
wa makampuni, mashirika na taasisi mbalimbali za umma na binafsi
zinazochangia kwa kiasi kikubwa mahitaji na hata majanga yanapotokea ili
kunusuru na kuboresha maisha ya watanzania wenzetu na kuthamini
michango na misaada yao,”alisema.
Alisema mfumo huo unaoaznishwa
una lengo la kutambua michango na misaada mbalimbali inayotolewa na
wadau kwa jamii pia wadau nao wapate fursa ya kuweka malengo yao ya
uwajibikaji kwa jamii kwa kuona ni wapi wanaweza kuwekeza zaidi
kiuwajibikaji na eneo lipo nani amewekeza.
Shempemba alisema utafiti
walioufanya na kuutolea taarifa msimu ulipita kwa kushitikiana na
taasisi ya ukaguzi ya Konsalt inayofanyika kila mwaka wapo waliosaidia
jamii kwa sekta mbalimbali kama huduma za afya, maji, miundombinu,
elimu, michezo, maafa na mambo mengine kwa asilimia tofauti.
Aliongeza kuwa tafiti hizo pia
zimesaidia takwimu za misaada iliyotolewa kisekta, gharama zilizotumika,
uwajibikaji jamii ulivyowekezwa, jamii ilivyonufaika na misaada hiyo na
wadau walivyonufaika na uwekezaji wao kwa jamii hizo.
Post a Comment